Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, amedai kuwa chama hicho kimezuiwa kufanya mkutano wake uliopangwa kufanyika leo, Februari 27, 2025, katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam.
Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa X, Lema amesema walipata taarifa kuwa ukumbi waliokuwa wameukodi hauwezi kutumika kwa sababu ya hitilafu ya umeme na AC. Baada ya kuelekezwa kwenye hoteli ya Coral Beach kama mbadala, nao walizuiwa baadaye na menejimenti ya hoteli hiyo.
Lema ameitaja hali hiyo kuwa ni aina ya ubaguzi, lakini ameahidi kuwa CHADEMA haitakata tamaa. Mkutano huo sasa utafanyika katika Makao Makuu ya chama kuanzia saa 12:00 jioni leo.
Soma, Pia: Godbless Lema watangaza kufanya tukio kubwa Tarehe 27 Februari, 2025 ikiwemo kuzindua kampeni ya kidigitiali
Andiko la Lema kutoka X (zamani twitter);
"Tulikuwa Tumefanya Booking ya Ukumbi kwa ajili ya shughuli yetu leo 27/2/2025 ktk hotel ya Sea Clif Hotel. Asubuhi nilipigiwa simu nikaambiwa kuna dharura kuwa AC zimeharibika na umeme umekoroga hapa ukumbini na kwa hiyo hatuwezi kufanya mkutano wetu, Sea Cliff wakatutafutia ukumbi mbadala ktk hotel ya Coral beach."
"Tulienda Coral beach hotel na kukubaliana tutafanyia hapo na maandalizi yalianza. Baada ya masaa mawili nikipapigiwa simu kutoka kCoral beach kwamba wamepokea meseji kutoka menejimenti ya juu kuwa CHADEMA hawaruhusiwi kufanya mkutano hapo.
"Hii mbegu ya ubaguzi waliyopanda wataijutia sana. Hata hivyo hatuwezi kukata tamaa hivyo basi tumeamua kuwa tutaendelea na tukio letu kama lilivyopangwa ktk ukumbi wetu Makao Makuu ya Chama kuanzia saa 12:00 Jioni. Wanachama wote na waalikwa karibuni. Defeat is not an option."