Kwa hali hii wanaume lazima tufe mapema!..

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
8,313
Reaction score
12,170
Jamaa kaamka asubuhi, kavaa track suit na kumuamsha mkewe!.

MUME: Amka twende jogging mke wangu?
MKE: Alaaa kwa hiyo una maana mie tipwatipwa?

MUME: Hapana si hivyo jogging ni nzuri kwa afya.
MKE: Kwa hiyo una maana mi mgonjwa?

MUME: Basi yaishe endelea kulala
MKE: Kwa hiyo unaniona mi mvivu sana sio?

MUME: Hujanielewa mpenzi wangu sikuwa na maana hiyo baby.
MKE: Kwa hiyo mie mjinga mpaka nashindwa kukuelewa?

MUME: Jamani mi sijasema hilo
MKE: Kwa hiyo mie muongo?

MUME: Chonde tusiendeleze haya asubuhi namna hii
MKE: Kwa hiyo mie ndio naendeleza ugomvi?

MUME: Sikia we lala mie naenda jogging.
MKE: Ndio zako hizo mambo yote unafanya peke yako hunishirikishi"

MUME: Unajua nimeanza kusikia kizunguzungu
MKE: Unaona nikiongea kidogo unakimbilia kuumwa, mbinafsi sana wewe..

MUME: Basi ngoja tu nilale siendi jogging
MKE: Kwahiyo ulikua unanijaribu?

Wanawake Mungu anawaona 😀😀

NDIO MAANA WANAUME TUNAKUFA MAPEMA NA KUWAACHA WENGI MKIWA WAJANE
⚰⚰⚰
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…