Ushamba mtupu kuanzia stage yenyewe mpaka hao wasanii na watangazaji.
Tunahitaji a lot of improvement ili tuweze kuwa serious kwenye hii award. Jamani angalieni wenzenu wanavyotengeneza mipango yao na nyinyi mujifunze kutoka kwao. Jana usiku hata hao wasanii kuwaona kwenye stage ilikuwa mpaka urekebishe eyesight yako.
Hao wasanii hawajui kuvaa kabisa na hasa kweenye function kama ile. Msanii anakwenda pale na kikofia chake kimeandika NY (New York) pamoja na sunglasses (za kike na kiume) maana yake nini? Haoni au imekuwa vipi? Baadhi yao kuimba live wameshindwa kabisa nadhani kutokana na kukosa uzoefu.
Nyimbo nyingi hazieleweki hata kile kinachoimbwa (booooooring!). Ambazo nimeona angalau zina mwelekeo zilikuwa 'habari ndiyo hiyo', ile ya msondo ngoma pamoja na ya 'njiwa'.
Maoni yangu:
Inatakiwa wale watakoimba wafanyishwe mazoezi kabla ili kuangalia mambo yatakwenda vipi.
Kuwe na taasisi ambayo inawapa mafunzo hawa waimbaji na waigizaji vijana na wazee heshima zinazohitajika pindi unapokuwa kwenye hadhira kama ile. Wenzao Marekani huwa wanakwenda hizo shule special kwa ajili ya mafunzo hayo.
Uchaguzi wa nyimbo: asilimia 60 iwe kutoka kwenye kura za wananchi na 40 kutoka kwa wataalamu wa fani hiyo. Kwa mfano, nimeshangaa kuona msanii kama Mjomba amekosa tuzo na amepata Mpoki, lakini ukiangalia hasa utaona mantiki na utunzi wa mjomba uko makini zaidi.