Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Kiukweli tangu mwaka huu uanze kumekuwa na utitiri wa matukio ya mauaji na utekaji ambayo hakuna hata moja tumepatiwa majibu.
Tukio likitokea, formula ni ile ile. Polisi watatoa "Statement" kwenye social media alafu mwishoni utakutana na sentesi ya UCHUNGUZI UNAENDELEA.
Ni kama Polisi kazi ya uchunguzi either imewashinda au hawataki kutwambia walichochunguza!
Ndo maana ni muda sasa iundwe taasisi huru ambayo itajihusisha na UCHUNGUZI PEKE YAKE.
Hiyo taasisi inakuwa kama TAKUKURU au TRA. Polisi kazi yao inakuwa ni kukamata lakini Uchunguzi unafanywa na hiyo taasisi ambayo napendekezwa iitwe TANZANIA BUREAU OF INVESTIGATION (TBI)
Ukweli ni kwamba Polisi hawawezi kujichunguza wenyewe na pengine wana majukumu mengi kwa hiyo wakipunguziwa mambo yataenda kwa haraka zaidi.
Haiwezekani kesi ya Lissu, Sativa, Ali Kibao, Ben Saanane, Deusdedith Soka n.k zote zisiwe zimepatiwa majibu hadi sasa.
We need the Tanzania Bureau Of Investigation. Kama mmeweza kutengeneza TAKUKURU na TRA hata hili pia linawezekana.