Kwa hali ilivyo ni vyema ziwekwe wazi taraatibu za kufuatwa na vyombo vya usalama kabla ya kumkamata mtuhumiwa

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
Nadhani isishie kujitambulisha tu au kuelezewa kosa lako tu ila tuende mbali kidogo pawepo na mashahidi /kiongozi wa mtaa, ifamike hao wana usalama ni wa kituo kipi na waache vielelezo na wana elekea wapi na mtuhumiwa.

Kujitambilisha sisi ni askari istoshe raia kurusu mpendwa wao kuondoka , ni vyema kama mtu hajaacha vielelezo vitakavyo saidia pindi mtuhumiwa atavyofikwa na changamoto basi mtu ajiokoe hata kwa kupiga yowe au kukataa kuondoka .

Au ufuatwe utaaratibu wa kumtaka mtuhumiwa afike kituoni na notice hiyo akabidhiwe yeye na ndugu zake wa karibu.

Kuna uwezekano vyombo vyetu vya usalama kuchafuliwa kwa matukio ya aina hii hivyo ni vyema vyombo hivi vituweke sawa pia tutawatofautishaje na watekaji na wauaji.

Natambua kuna watu wengi sana washadanganyika kwa mtindo huu hivyo ni vyema raia tupewe taaratibu rafiki na salama.

Muwe na siku huku tukiburudika na wimbo wa lucky dube --- crazy world
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…