Kwa hali niionavyo uwanja wa mkapa muda huu, upo uwezekano wenye tiketi waliopo nyumbani wakakosa viti

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Mm nna uzoefu na uwanja wa mkapa, sana tena, hiki nachokiandika nimewahi kukutana nacho mara tatu, umekata tiketi ya shs 20,000/= unaenda uwanjani saa 9 unakuta VIP B imejaa na huna siti ya kukaa.

Kitendo cha kufungua mageti saa 2 ni kizuri lakini nna uhakika wahuni wengi wataingia kwa shs 3000 had shs 2000, wakifika ndani wanacheza mchezo wa kutoa elfu 3 wanaenda mahali ambako sio siti zao.

Ukweli ni kuwa siti za VIP B na C zinakaliwa na wahuni ambao hawakukata tiketi, nimelalamikia sana jambo hilo lakini hadi Leo nimedharauliwa.Kama nadanganya nendeni kwenye siti za VIP B na C mtaona watu wachafu, wamevaa kandambili lakini wamezamia kwenye majukwaa yasio ya status zao.

Kama wewe ni mshabiki umekata tiketi ya maeneo ya VIP B na C na hadi sasa hujaenda uwanjani, ujue umekwisha.Ikifika saa 10 hakuna siti tena
 
Mtajuana wenyewe na siku yenu
 
Acha uongo..tiketi hatujakata...Viongozi wamazinunua na kuzigawa matawini ...ili tuujaze uwanja...

Rage alikuwa mkweli..
 
Mkuu kwa hiyo kuvaa kandambili ni disqualification ya kukaa VIP?!
Umezingua sana.
 


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani wenye wivu wajinyongeeee leo ni motooo....yani unyamaa ni mwingiiii
 

Hapo kwenye wa chafu na wavaa kandambili unakosea watu kwaiyo izo siti ni za watu wanaovaa viatu na usafi tu jiangalie wewe unaweza ukawa hujui kuvaa uko rafu ila mpunga upo usikariri maisha shubaamit zako… nawatetea tu watani wangu shubaamit zako
 
Kwenye uvaaji hapo umechemka Kuna watu uvaaji sio kipaumbele kwao ila hela kama hiyo ya kawaida hawakosi
Halafu wengine wanapenda position ili afurahie mchezo kwa hiyo anakaa mahali pazuri bila kujali sana kiingilio.
 
Wote tiketi mmepewa sasa usishangae kumkuta shabiki kavaa kandambili VIP.
Tiketi za 5000/= zinaruhusu ayo kutokea istoshe nyote ni mashabiki wa mbumbumbu fc.
 
Acha dharau mkuu [emoji28] kwahiyo Sisi wavaa kandambili hatuwezi kumudu tiketi ya elfu kumi sio??
 
Hiki kitu ndio hasa kilinifanya niachane na Mpira wa uwanjani nikaangalie Bar. Upuuzi kabisa unalipa kiingilio kikubwa unakosa siti, Bora kuweka heshima bar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…