Dumelambegu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 1,052
- 257
Kwa maoni yangu, hali ya muungano inaendelea kuwa mbaya. Wanaosema muungano ni imara ni viongozi tena wa chama fulani. Chuki ya wananchi wa pande hizi mbili inaendelea kukua. Sasa kwa mwenendo huo nawaonya viongozi wa hicho chama fulani wasije wakalogwa na kusema sasa ni zamu ya visiwani, wataangukia pua na watajuta. Siasa za nchi hii chini ya uongozi wa sasa zimekuza ufa kati ya bara na visiwani. Wabara hawatakubali kudanganywa tena.
Tanganyika wameitawala Zanzibar kwa miaka yote hii na tulivumilia.
Sisi tumeanza kulalamika kwa tunaloliamini, sioni sababu kwanini na nyinyi msonyeshe hisia zenu.
Hata hivyo, ingekuwa vyema mkadai Tanganyika yenu kuliko kutoa misimamo hii msioweza kuisimamia.
Ni ushauri tu Wakuu.
Sasa kama Tanganyika haipo, tunatakiwa tuidai Tanganyika yetu, ni wakati gani ambao Tanganyika ilitwala Zanzibar? Think between the line. Ukweli unabaki kuwa Wazanzibari wameendelea kushika nafasi kwenye serikali ya muungano na kuwatawala watanganyika, lakini watanganyika hawana nafasi yoyote kwenye utawala wa serikali ya Zanzibar
Kwetu sisi hakuna tofauti baina ya Tanzania yenu mnayoiamini na Tanganyika yenu mlioiua.
Tuliposema daini Tanganyika yenu namaanisha muandike Katiba ya Tanganyika itakayowaondoa Wazanzibari wanaoshika hizo nafasi zinazowatoa roho zenu.
Watanganyika wapate nafasi gani za utawala wa Zanzibar wakati utawala wenu wa kivamizi upo?
Nyie vipi?