Kwa haya aliyoyafanya, Polepole hapaswi kuitwa Mzalendo

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Katika taifa hili mtu ukifikiria sana unaweza weka kuona ni unafki mtupu umetamalaki kila mahali, yaani ni umbeya tu na Majungu ndiyo maisha yetu ya sasa.

Yaani Polepole huyu aliyekua anawasiliana wenzake hadharani akiwa mwenezi wa ccm? Huyu huyu Pole pole ambaye alikua ambaye juzi juzi tu anatambia wenzake kua CCM inatumia magari ya kifahari aina ya V8?

Huyu huyu Humphrey Polepole aliyeongoza movements za katiba mpya enzi za JK iliyotumia mabilioni ya pesa na baadae akageuka akasema katiba haina umuhimu?

Huyu huyu Polepole aliyeshiriki kuandaa uchaguzi haramu wa serikali za mitaa 2019 na ule wa 2020 wakafanya hujuma CCM ikapitisha watu wake kila mahali eti bila kupingHuyu

Huyu huyu Polepole aliyekua akifurahia kupigwa Risasi Tundu Lissu. Eti ni mzalendo! Khaaa! Hebu nipisheni nipite mie.

Tujue kutofautisha uzalendo na Kinyongo cha mtu. Polepole hana uzalendo wowote, ni kinyongo dhidi ya uongozi wa awamu ya 6, hakubaliani na uongozi wa Mama hili lazima tuliseme wazi.

Kuondoka kwake JPM hakutarajia kabisa maana aliona ndiyo taa ya maisha yake binafsi. Mtu kigeugeu huwezi kumuita mzalendo zaidi ya mnafki.
 
Kawashika kunako sasa mna bweka.

Polepole kamatia hapo hapo.

Mmabo ya Parallel Government yapo awamu hii kwa sana tu.
 
Msoga gang mpo overrated.

Eti hapa na nyie mmekaa mkafikiria hadi mwisho!

#kataawahuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…