Kwa haya ni kweli kabisa Watanzania walilishwa Limbwata

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Naweza amini kabisa pasipo shaka kwamba Watanzania tulilishwa limbwata na hilo limbwata huenda lilichukuliwa sayari tofauti na hii make nimejaribu kufukunyua nchi zenye tabia kama zetu nimekosa kabisa Dunia nzima.

Na hivi ni viashiria kwba tulilishwa limbwata:

1. Pesa za umma zinapigwa na sisi tuna fanya joking, yaani the more upigaji unavyo pamba moto ndio the more joking zinavyo pamba moto, hii sio tabia ya kawaida ni Limbwata, yaani tunawashingilia wanao poha pesa za umma.

2. Wafanyakazi wanaweza wasiongezewe mishahara na masilahi mengine hata miaka 10 na hakuna wanacho weza kufanya sana sana watalalamika wakiwa kwenye vijiwe vyao basi.

3. Ni nchi pekee hadi Profesor ili aishi lazima ajipendekeze, yaani unakuta kapiga kitabu sana tena nje ya nchi but Survive model yake ni ya kujipendekeza tu,na kuabudu, Hili ni limbwata

4. Ni nchi pekee ambayo akili zimewekwa pembeni na raia wanaishi ki ujanja ujanja na kujikomba, levo za kujipendekeza zinatofautiana.

4. Wabongo wanaweza tukanwa na watawala na hakuna kitu wanaweza fanya zaidi ya kunung'unika, angalia Mwigilu na Nape wanavyo wakejeli wabongo, hii haiwezi tokea kwingine kokote kule zaidi ya Tanzania tu.

5.Watanzania huanza kutoa rushwa kabla ya kuombwa rushwa, yaani wanajipeleka kwenye mdomo wa Mamba wenyewe na baadae wanaanza kulalamika.

6.Ubunge ni Ajira tosha kabisa, na pale Bungeni ni kituo cha kwenda kuabudu na kusifia watawala.

7.Tanzania ndio nchi pekee chini ya Jua ambako Wageni huwanyanyasa na kuwabagua wenyeji ndani ya nchi yao, Hili huwezi kutana nalo kokote kule, angalia wakina Kanjibay na wale macho madogo wanavyo nyanyanyasa Wabongo na hakuna kitu tunaweza wafanya.

8.Wabongo wanaweza lipishwa nauli kwenye basi na Basi likifika kwemye mizani wana chuchumaishwa eti uzito usizidi unakuta Dingi lina watoto lina chuchumaishwa, hii ni zaidi ya Limbwata.

9.Wabongo ndio hushukuru mtoa huduma badala ya mtoa huduma kuwashukuru wao, huu ni uzezeta na ulimbawata mkubwa sana.

10. Bongo Elimu ni Biashara, shule ina michango zaidi ya 15 plus ada, sasa jiulize Ada kazi yake ni nini kama.unatoa ada na bado unatoa tena mara pesa ya chakula, nini kazi ya pesa ya Ada? na hakuna mtu analalamika.

11.Wabongo wameaminishwa kwamba elimu bora ni mtoto apate max zote, au afaulu mtihani bila kujalisha hapo shuleni anatoka na kitu gani cha kumsaidia mbeleni, Wabongo wanaabudu matokeo ya mitihani kuliko uwezo binafisi wa mtoto, huu ni Ulimbwata.

12. Mbongo anaweza lalamikia huduma mbaya na still akaendelea kuitumia hata kama kuna mbadala wake, huu ni uzezeta na Ulimbwata.

13. Ni Tanzania ndio nchi pekee raia huchangishwa.michango ya kujenga mara shule mara Hospitali ilihali wanalipa kodi kila siku, huu ujinga hauko kokote kule zaidi ya kwenye nchi ya walio lishwa limbwata.

14.Tanzania ndio nchi pekee raia hujivunia products za nchi nyingine, unaweza kuta raia anajivunia Yutong za Kichina utazania nchi yake ina Hisa kwemye kiwanda kumbe hakuna ni ujing ujinga tu.

15. Tanzania umasikini ni mtaji namba 1 wa watawala kuendelea kutawala, yaano ili watawala waendelee kutawala ni lazima umasikini uendelee kuwepo, umasikini mtaji wa kisiasa hasa kipindi cha kampeni.

Unaweza Ongezea zingine ila kwa kifupi Limbwata lipo na tulilishwa na alie tulisha hajulikani.
 
Utaumiza kichwa bure. Bongo ni free race Hakuna staili maalumu ya kuishi. Ishi vyovyote utakavyo. Nchi ipo autopilot failure state.
 
step inayofata failed State .mpaka leo moderate na mlaumu sana uzi wangu alifuta niliota 2025 maamuzi yatakuja kufanywa na jeshi.
 
Tofautisha kati ya limbwata, na kurogwa!! Sisi tumerogwa. Yaani unaona kabisa unaonewa, lakini unachagua kuvumilia, badala kuchukua hatua dhidi ya hayo mambuzz.
 
Ningependa sana kama ungetumia ujinga na si limbwata,,.Hii Nchi ina ujinga mwingi sana ambao upo ndani ya mioyo yetu..
 
Namba 4.b /5??🤣🤣

Yani jamaa anasimama bila aibu anasema hakuna mTu atagongewa mlango alipe deni la taifa

Aisee 🙌
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…