benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
"TUJIKUMBUSHE KIDOGO"
Mwanzoni mwa mwaka huu, mwezi Januari, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe aliagiza mtuhumiwa aliyekuwa amekamatwa kwa kosa la kuendesha kiwanda bubu cha kutengeneza mafuta ya Mawese katika Kijiji cha Kongowe-Kibaha, Halifa Said atafutwe na asaidiwe na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO). Awali Halifa alikamatwa na Polisi kwa tuhuma za kuendesha kiwanda Bubu lakini Waziri Bashe alisema Serikali ya Rais Samia inapaswa kuwezesha wananchi na sio kuwa Serikali ya kamatakamata na fungiafungia
Siku chache zilizopita akiwa Kijiji cha Ugaka, Waziri wa Nishati, January Makamba akizungumza katika mkutano wa hadhara alizungumza na mwananchi Shaban Ali ambaye kwa sasa anafanya biashara ya mafuta kwa njia ya chupa na madumu kwenye Kijiji hicho ambapo alisema Serikali itamkopesha Shilingi Milioni 50 kutoka katika Shilingi Bilioni 2 ambazo zimetengwa na Wizara kama sehemu ya majaribio kwa mwaka huu wa fedha kuwawezesha Wajasiriamali kufungua vituo vidogo vya mafuta vijijini ili kuuza mafuta safi, kwa njia salama na kwa bei elekezi.
Kwa mara nyingine tena, ingekuwa ni Serikali ile iliyopita huyu kijana angekuwa anapumulia nyuma ya nondo kwani badala ya kumuwezesha angeanza kuulizwa leseni ya biashara, cheti cha TBS, NEMC wangekuja kudai EIA na mambo mengine kibao ya kukwamisha biashara.
Bashe na January ni mfano tu wa yale anayoyahubiri Rais Samia Suluhu Hassan lakini hii haipaswi kuishia kwa mtu mmojammoja bali mifumo imara na thabiti inapaswa kuwekwa ili haya wanayoyafanya yawe endelevu hata pale watakapoondoka katika nafasi walizopo hivi sasa.
Ila yote kwa yote nyakati zimebadilika sana.