MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nimetafakari sana nimeona hii demokrasia tunayolazimishwa kuifuata inazidi kutudidimiza. Iko kinyume kabisa na shughuli za maendeleo. Mabeberu waliona mbali sana kwa kutuaminisha kuwa WENGI WAPE. Na kuna wengine wana msemo wao wenye utata usemao "Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu"... binafsi sioni lazima ya WENGI WAPE ikiwa hao wengi hawana hoja nzito za kisayansi mezani.
Kwa mfano wafuasi wa Mwamposa, Kiboko ya wachawi, Kuhani Musa, Mkandamizaji, na manabii feki wengine ni wengi sana kiasi kwamba wana madhara kwenye sanduku la kura. Sasa kwa uwingi wao si wanaweza wakasababisha tukapata kiongozi mbovu kisa tu wengi wape?
USA waliona mbali sana ndo maana kwenye uchaguzi wao kuna kikundi cha watu wasiozidi 600 huamua nani awe Rais kwa kupiga kura baada ya wananchi wote kupiga kura. Yaani wananchi hata kama mlimchagua kiongozi wenu ni kuwa hicho kikundi ndo kina kauli ya mwisho nani awe Rais. UK na mfalme wao hawana muda na demokrasia za kipuuzi. Waarabu na wachina nao hawana huu ujinga tulio nao.
Pia kwenye hii demokrasia yetu tunatumia muda mwingi sana kwenye mijadala na kubishana badala ya kufanya maendeleo.
Kimsingi maendeleo hayahitaji kumbelezana wala mijadala mingi. Ninashauri Afrika tuamue jinsi gani ya kufanya mambo yetu bila kufuata hii demokrasia uchwara.