Kwa hii rasimu ya katiba nahisi tutaibua mgogoro mwingine wa kikatiba

Kwa hii rasimu ya katiba nahisi tutaibua mgogoro mwingine wa kikatiba

mnyikungu

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2009
Posts
1,962
Reaction score
2,477
wapenda wana JF hii rasimu ya katiba kweli ni nzuri ila kuna mambo kama mabaraza ya katiba yasiporekebisha na ikapita hatimaye ikaleta katiba mpya basi utsatokea mgogoro wa kikatiba
moja kati ya mambo hayo ni huu mfumo wa serikali tatu, mimi siyo mtaalam wa sheria lakini kwa hili nahisi litatengeneza mgogoro wa kikatiba. wanasema kuwe na serikali tatu yaani ya muungano ya tanzania bara na ya zanzibar, sasa tujiulize je hiyo rasimu ikipitishwa na kuwa katiba ni lini itaanza kutumika? je itatumika kabla ya katiba ya tanzania bara au ya tanzania bara itafuata?
kama itatumika kabla ya katiba ya tanzania bara hapa ndo mgogoro utapoanzia, ikiwa katiba inatambua uwepo wa serikali tatu itakuwa na uhalali gani wa kutumika wakati serikali moja haipo? je hiyo rasimu imeitoa wapi hiyo tanzania bara? je nchi yetu ta tanganyika tukiirudisha kwa jina letu la Tanganyika itatambuliwaje na katiba ya muungano wakati tiyari hiyo katiba itakuwa inaitambua tanzania bara? je hiyo rasimu ikipita na kuwa katiba ina uhalali gani wa kuitambua nchi ambayo haipo? haya tukishatengeneza katiba yetu mtangayika atakuwa ni nani? je ni mambo gani yatakuwa ya tanganyika na mengine ya muungano? na je hayo mamlaka ya katiba ya muungano imeyatoa wapi wakati katiba ya tanganyika haipo? na hatujuia kama hiyo katiba itaukubali muungano au la? na je ikitokea katiba ya tanganyika haikubaliani na mambo fulani ya muungano kitatokea nini?

KUNA MAMBO MENGI YA KUHOJI KABLA YA HII RASIMU YA KATIBA KUPITISHWA, SWALI JE HAYO MABARAZA YA KATIBA YATAYAONA HAYA? PIA HII RASIMU KUNA VIPENGELE VITAHAMASISHA UUAJI, MFANO PALE INAPOSEMA MGOMBEA KUTOKA CHAMA CHA SIASA AKIFA BASI NAFASI YAKE ITAJAZWA NA CHAMA CHAKE BILA KURUDIA UCHAGUZI, HATU0ONI HAPA TUTAUWANA BILA SABABU?, HEBU FIKIRIA MTU KAMA FILIKUNJOMBE ( MFANO TU) HAKUBALIKI KWENYE CHAMA CHAKE NA SASA HIZI WANASHINDWA KUMFUKUZA AU KUMFANYA CHOCHOTE MAANA HAINA MAANA KWAO NA WANAHOFIA WAKIRUDI KWENYE UCHAGUZI WANAWEZA KUPOTEZA JIMBO KWA UPINZANI, SASA KWA HUU MFUMO MPYA WATAKUWA HAWANA CHA KUHOFIA MAANA HATA AFE JIMBO LINABAKI KWAO JE HATUONI KUWA HUU UTARATIBU UTASABABISHA VYAMA VIWE VINAPANGA NJAMA HATA ZA KUWAUWA WALE WABUNGE AMBAO HAWAKUBALIANI NAO ILI KUWAWEKA WATU WAO?
KWA SELIKALI TATU KWAHERI MUUNGANO KARIBU TANGANYIKA. NAOMBA KUWAKILISHA
 
baregu na wenzake nusu wazima nusu akili zao zina mushkeli au wameiandika rasimu wakiwa magogoni chini ya mtutu wa bunduki..kumpa rais hayo madaraka yote ya uteuzi ni kuminya uhuru(especially wa mahakama)
 
kama vile hawaujui mhimili wa mahakama ulivyo
 
yatafanyiwa kazi tuu maana sasa inaandikwa katiba ya jamhuri ya muungano sio ya bara sasa ikipishwa kuwa katiba halisi hapo mwakani kuna mawili au tuandike katiba ya bara haraka haraka iwahi uchaguzi au uchaguzi ufanyike then mamlaka ya bara iwe chini ya rais wa muungano kwa muda wakati tunaandaa katiba na uchaguzi! maana hii ni rasimu tuu haijapishwa so isngeweza kusema chochote kuhusu Tanganyika na namna ya kuianzisha!!
 
ni kweli usemacho ila swali langu je hii rasimu ya katiba ikipita itakuwa na uhalali gani wakati serikali moja haipo na yenyewe inatambua uwepo wa serikali tatu?
 
Na endapo rais wa muungano ni mzanzibari je atatawala bara?
 
baregu na wenzake nusu wazima nusu akili zao zina mushkeli au wameiandika rasimu wakiwa magogoni chini ya mtutu wa bunduki..kumpa rais hayo madaraka yote ya uteuzi ni kuminya uhuru(especially wa mahakama)
Dau limepanda sasa toka book 7 mpaka buku kumi amekuwa baregu, sio warioba kakiuka maccm mulichomtuma nini kachukua ya wananchi, sasa fanyeni kampeni za kubadirisha kwa busara mukianza kupick wajumbe badala ya mwenyekiti katiba hamuoni 2014 kwa sababu munataka kutumia utapeli badala ya hoja
 
baregu na wenzake nusu wazima nusu akili zao zina mushkeli au wameiandika rasimu wakiwa magogoni chini ya mtutu wa bunduki..kumpa rais hayo madaraka yote ya uteuzi ni kuminya uhuru(especially wa mahakama)

mkuu umepatia sioni maana ya huu utumbo ni sawa mbwa kumwita jibwa katiba ni ile ile sawa na soda kubadilishwa chupa tu
 
Ili kuijenga katibu iliyo bora na nzuri wajibu wetu sote ni kusaidia kuboresha maoni na ikiwezekana badala ya kuonesha mianya ya udhaifu wake pekee, tujikite zaidi katika kutoa utatuzi wa mianya/madhaifu hiyo/hayo mapema.

Wazee wetu hawa hatupaswi kuwalaumu moja kwa moja kwani kazi waliyoifanya inatosha sana na imebaki kazi moja tu kwa umma wa watanzania wote kushiriki kwa kufuata adidu rejea hiyo na hatimaye waitimishe zoezi zima kwa manufaa ya nchi.
 
wapenda wana JF hii rasimu ya katiba kweli ni nzuri ila kuna mambo kama mabaraza ya katiba yasiporekebisha na ikapita hatimaye ikaleta katiba mpya basi utsatokea mgogoro wa kikatiba
moja kati ya mambo hayo ni huu mfumo wa serikali tatu, mimi siyo mtaalam wa sheria lakini kwa hili nahisi litatengeneza mgogoro wa kikatiba. wanasema kuwe na serikali tatu yaani ya muungano ya tanzania bara na ya zanzibar, sasa tujiulize je hiyo rasimu ikipitishwa na kuwa katiba ni lini itaanza kutumika? je itatumika kabla ya katiba ya tanzania bara au ya tanzania bara itafuata?
kama itatumika kabla ya katiba ya tanzania bara hapa ndo mgogoro utapoanzia, ikiwa katiba inatambua uwepo wa serikali tatu itakuwa na uhalali gani wa kutumika wakati serikali moja haipo? je hiyo rasimu imeitoa wapi hiyo tanzania bara? je nchi yetu ta tanganyika tukiirudisha kwa jina letu la Tanganyika itatambuliwaje na katiba ya muungano wakati tiyari hiyo katiba itakuwa inaitambua tanzania bara? je hiyo rasimu ikipita na kuwa katiba ina uhalali gani wa kuitambua nchi ambayo haipo? haya tukishatengeneza katiba yetu mtangayika atakuwa ni nani? je ni mambo gani yatakuwa ya tanganyika na mengine ya muungano? na je hayo mamlaka ya katiba ya muungano imeyatoa wapi wakati katiba ya tanganyika haipo? na hatujuia kama hiyo katiba itaukubali muungano au la? na je ikitokea katiba ya tanganyika haikubaliani na mambo fulani ya muungano kitatokea nini?

KUNA MAMBO MENGI YA KUHOJI KABLA YA HII RASIMU YA KATIBA KUPITISHWA, SWALI JE HAYO MABARAZA YA KATIBA YATAYAONA HAYA? PIA HII RASIMU KUNA VIPENGELE VITAHAMASISHA UUAJI, MFANO PALE INAPOSEMA MGOMBEA KUTOKA CHAMA CHA SIASA AKIFA BASI NAFASI YAKE ITAJAZWA NA CHAMA CHAKE BILA KURUDIA UCHAGUZI, HATU0ONI HAPA TUTAUWANA BILA SABABU?, HEBU FIKIRIA MTU KAMA FILIKUNJOMBE ( MFANO TU) HAKUBALIKI KWENYE CHAMA CHAKE NA SASA HIZI WANASHINDWA KUMFUKUZA AU KUMFANYA CHOCHOTE MAANA HAINA MAANA KWAO NA WANAHOFIA WAKIRUDI KWENYE UCHAGUZI WANAWEZA KUPOTEZA JIMBO KWA UPINZANI, SASA KWA HUU MFUMO MPYA WATAKUWA HAWANA CHA KUHOFIA MAANA HATA AFE JIMBO LINABAKI KWAO JE HATUONI KUWA HUU UTARATIBU UTASABABISHA VYAMA VIWE VINAPANGA NJAMA HATA ZA KUWAUWA WALE WABUNGE AMBAO HAWAKUBALIANI NAO ILI KUWAWEKA WATU WAO?
KWA SELIKALI TATU KWAHERI MUUNGANO KARIBU TANGANYIKA. NAOMBA KUWAKILISHA

Mimi nadhani kwanza hujasoma hiyo rasimu, na kama umesoma hujaelewa. Tatizo kubwa la watanzania ni kufikiria kuwa mambo hayawezekani hata kabla hawajajaribu. Ukiangalia maswali yako yote, japo mimi sio mwanasheria, sioni swali ambalo linaleta mgogoro wa kikatiba hapa. Nitakusaidia kukufafanulia
Katiba itaanza kutumika mara baada ya kupitishwa na wananchi. Tukichukulia mfano wa nchi ambazo zimetunga katiba mpya, kunakuwa na chomba cha kusimamia utekelezaji wa katiba mpya. Hata hivyo, uchaguzi mkuu mpya ndio unasababusha kutumika kikamilifu kwa katiba mpya kwa sababu, raisi wa sasa ameapa na katiba ya zamani, ila raisi anayekuja anaapa kwa katiba mpya. Ndio mana Kenya kwa mfano, walikuwa na waziri mkuu, hawakuwa na magavana, hawakuwa na naibu naisi lakini baada ya kuapishwa Uhuru Kenyata kuwa raisi mpya, katiba mpya imeanza kutumika vizuri zaidi hata ukaona hawana cheo cha waziri mkuu, wana magavana nk.
Kwani nani kakuambia kuwa katiba mpya itaanza kutumika kabla serekali ya tatu, yaani ya Tanganyika haitakuwepo?
Je hiyo rasimu imeitoa wapi hiyo tanzania bara? Kwani wewe leo ndio mwanzo kuona neno Tanzania bara? Kimsingi, baada ya muungano, neno Tanganyika lilikuwa halitumiki, bali Tanzania bara. Neno Tanganyika limetumiwa na watu wachache, kama Tanganyika law society nk. kwa hiyo usiwalaumu wajumbe wa katiba sana, japo kama Mtikila anavyosema, huenda likafufuliwa na wewe mwenyewe ukiungana kwenye mapambano ya kulitafuta jina Tanganyika, ambalo kimsingi mimi jina is not a big deal, tutalipata.
je hiyo rasimu ikipita na kuwa katiba ina uhalali gani wa kuitambua nchi ambayo haipo? Hili ndilo swali ambalo limenichekesha sana. nani aliyekuambia kuwa kuna nchi ambayo haipo? Na kama haipo nani aliyekuambia haitakuwepo? Mwaka juzi tu watu waliamua kutengeneza mipaka na South Sudani ikawepo, iweje ya Tanganyika ambayo mipaka yake ipo na inajulikana kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita.
Haya mawili ni ya ajabu, siyajibu.
Na je ikitokea katiba ya tanganyika haikubaliani na mambo fulani ya muungano kitatokea nini? Kwanza nikukumbushe tu kuwa watu wanaokubaliana kuungana sio kuwa wanakubaliana mambo yote. Hata mke wako au mume wako, sio kweli kama unaweza kukubaliana naye mambo yote. Ila kuna mbinu za ku harmonise yale ambayo hamkubaliani. Na huwa suala la katiba ni endelevu, ndio mana hata hii katiba tuliyo nayo imeshafanyiwa mabadiliko mara nyingi. Endapo kuna jambo ambalo limepitwa na wakati, linaondoewa na mengine yanaongezwa. Kwa hiyo, katiba itafanyiwa marekebisho ili iendane na katiba ya muungano au washirika wa huo muungano.

haya uliyoyaandika kwa maherufi makubwa sio ya maana kwa sababu unadhani kuwa watanzania ni wajinga kwa hiyo hawatayaona hayo mapungufu. Sio kweli hata kidogo, watanzania ni wajanja na lazima wapewe nafasi ya kujadili na kutoa maamuzi ya mustakabadhi wan chi yao.
 
Nafikiri kuna hoja ya msingi hapa!Tunatengeneza katiba ya nchi sio ya kijiji!
Inakuaje iseme sehemu moja kwamba Muungano ni kati ya iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar alafu sehemu nyingine iseme washirika wa muungano ni Tanzania bara na Zanzibar?Hii Tanzania Bara imetokea wapi?Katiba haitakiwi i'assume' tu kwamba inajulikana Tanganyika ndo Tanzania Bara.kwanini isi'assume tu pia kwamba Zanzibar ndo Tanzania Visiwani?kwani haijulikani hivyo?.........Kuna mambo mengi ya kujadili hapa....nitaendelea na comment baadae
 
Na endapo rais wa muungano ni mzanzibari je atatawala bara?

Haiingia akilini hata bila sheria au katiba mzanzibar aje awe rais wa Tanganyika au mtanganyika akawe rais wa Zanzibar!!
 
ni kweli usemacho ila swali langu je hii rasimu ya katiba ikipita itakuwa na uhalali gani wakati serikali moja haipo na yenyewe inatambua uwepo wa serikali tatu?

Serikali ya Tanganyika itakuwepo maana imeshatajwa kwenye katiba kitakachofuata ni muundo wake ambao unapaswa uwe ndani ya katiba ya Tanganyika!!ila serikali ya Jamhuri ya muungano imeridhia kuanzishwa kw Serikali ya Tanganyika ndani ya muungano isingeweza kwenda mbali na kuunda serikali hiyo na katiba yake hilo ni jukumu la Watanganyika wenyewe!!
 
Ili kuijenga katibu iliyo bora na nzuri wajibu wetu sote ni kusaidia kuboresha maoni na ikiwezekana badala ya kuonesha mianya ya udhaifu wake pekee, tujikite zaidi katika kutoa utatuzi wa mianya/madhaifu hiyo/hayo mapema.

Wazee wetu hawa hatupaswi kuwalaumu moja kwa moja kwani kazi waliyoifanya inatosha sana na imebaki kazi moja tu kwa umma wa watanzania wote kushiriki kwa kufuata adidu rejea hiyo na hatimaye waitimishe zoezi zima kwa manufaa ya nchi.

Ndugu yangu robert josephat, umeandika vizuri sana na ukizingatia pia wao nao uwezo wao wa kufikiri unachoka. Kimsingi wasiwasi wanachokifanya ni wajibu tu lakini matokeo yalishapangwa sidhani km huu mchakato kweli unaenda sawa na mawazo ya umma. Pili haya maswali ambayo wengi wetu tumekuwa tukijiuliza baada ya wao kuwasilish rasimu yao kweli hakuna hata mawili waliyokutana nayo wakati wa kukusanya maoni? Nikionacho hapa ni kudanganyana na kuchezea pesa za walipakodi. Sina imani sana na mfumo mzima wa zoezi hili kimsingi.
 
Muungano uliokuwepo ulikuwa waKarume na Nyerere, watanganyika au Wazanzibar hawajawahi kuulizwa na hata kuupitisha kwakura ya maoni. Si sawa kuhoji mazingira ya wakati ule ya vita baridi vyamagharibi na mashariki jinsi vilivyopelekea nchi mbili hizi kuungana kwa mtindohuo lakini ni vizuri kuungalia ni utaratibu gani nchi zinazoungana zinatakiwakuufuata mpaka kuingia katika muungano. Kabla na baada ya rasimu ya katibakuna mawazo mchanganyiko juu ya muungano, wengine (hasa Wazanzibar) wanaoneshadalili za kutaka kuuvunja, wengine wanautaka lakini wanatofautiana juu yamuundo wake. Kwa maana hiyo basi ilipaswa kwanza Watanganyika na wanzazibartutengane kwanza katika hii ndoa kwa muda (si kuachana) kwani ni kama mume namke mmekaa mkachokana, wakati mwingine mnaweza kuamua kwamba mtengane kwa mudana kutafakari yale yatokeayo katika ndoa yenu na baadaye mpime kama mrekebishekasoro zenu mweendelee au msiendelee; kwa njia gani? Kwa kuunda serikaliya mpito (ya muungano) ambayo itasimamia kwanza uundaji wa serikali yaTanganyika na pia kuipa mamlaka kamili Zanzibar kurekebisha katiba yao jinsiwapendavyo wenyewe katika mazingira yao ya kudai uhuru kamili. Baada ya katiba za nchi mbili(Tanganika na Zanzibar) kupitishwa na mabunge yao (Mabunge maalum ambayo kwaTanganyika yanaweza kuusisha wabunge wa bara waliopo) then wananchi wa kilaupande watapewa nafasi ya kutoa maoni kama wanataka kuingia jumuiya ya AfricaMashariki au wanataka kuungana na nchi gani si lazima hizi mbili tu kwani kamanilivyosema mwanzo mazingira sasa si yale ya vita baridi na hata kama nikuungana tena kwa maana ya Tanganyika na Zanzibar tena wanautaka muungano uwekatika mambo gani na mfumo upi?! Nashangaa kwanini tunawang'angania watumilioni moja kwa gharama kubwa za ajabu za serikali tatu ambayo kwa hakikaitabebwa na wadanganyika. Kama watasema hawataki muungano thenni kuamua kuwaacha ila napendekeza kuwa kama ilivyo kuwa mwaka 1961 baada yauhuru wananchi walioko upande wowote wa muungano wapewe uhuru wa kuchaguawanataka uraia wa upande gani, that is, kama mzanzibar amekaa Tanganyikamiaka mingi au mtoto kazaliwa Tanganyika na kukulia huku na akapima kama aweraia wa Tanganyika kwa maana kuwa makazi yao yako Tanganyika na kwa hivyoakaona bora awe raia wa Tanganyika aruhusiwe awe raia wa Tanganyika namtanganyika aliyeko Zanzibar naye atendewe vivyo hivyo. Kwa ujumla tunalazimisha jamboambalo limefikia mwisho wake kwani kwa mtazamo wangu rasimu hii haitakubaliwana wanzibar kamwe, wanachotaka wao ni Zanzibar huru, wajiunge umoja wa mataifa,wapate misaada na kujiunga katika taasisi zozote wazitakazo kama OIC nk naraisi wao atambulike, awe fastjet na yeye na kwa hakika kwa mtazamo wanguwataendelee sana kwani kwa misimamo ya dini yao hawajaharibika sana kuwamafisadi kama wadanganyika. Tutafakari, we have nothing to loose but they haveeverything to gain.
 
Back
Top Bottom