Kwa hili benchi la ufundi taifa stars mmewakosea watanzania

Jj football

New Member
Joined
Mar 8, 2018
Posts
4
Reaction score
8
Imekuwa Kasumba kwa makocha wa taifa stars kuchagua wachezaji wa timu ya Taifa kwa mazoea, hali hii inapunguza uzalendo wa kushabikia timu yetu ya taifa. Kila siku wadau wanajitokeza kuwapa ushauri ni jinsi gani tunaweza kuifikisha Taifa stars sehemu nzuri lakini ushauri wao haufanyiwi kazi.

Hivi unawezaje kumwacha mchezaji kama Rashid Mandawa kwenye timu ya taifa? Juzi tu kawafunga Township Rollers wapinzani wa Yanga magoli matatu pekee yake sio hivyo tu bado ameendelea kufanya vizuri ligi kuu ya Botswana hadi sasa amefunga magoli kumi na moja na anazidi kuipeperusha Bendera ya Tanzania vizuri nchini Botswana.

Wachezaji wengi wa Tanzania wanapotoka njee ya Tanzania wanakosa nafasi tena ya kuitwa timu ya taifa mfano Deogratius Munish na bado ana kipaji kikubwa na uzoefu wa mechi za kimataifa.

Ni vyema sasa benchi la ufundi la timu ya Taifa lifanyiwe maboresho kwa kuongeza watu wa kuscout wachezaji wetu wanaocheza njee ya nchi na kutafuta takwimu zao ili soka letu lipige hatua.

Naijeria kila mwaka wanaandaa mechi za ushindani kwa vijana wao waliopo njee ya nchi na cream wanayoipata wanaishindanisha na wachezaji wao wa ndani ndio maana kila siku wanafanya vizuri kuanzia timu za vijana hadi timu ya taifa.

Tuna wachezaji zaidi ya ishirini ambao umri wao ni chini ya miaka 21 ambao wapo njee ya nchi kwenye academies kubwa kama Aspire, Reading , lassenCcSoccer,Vancouver whitecaps, Sc Heerenveen na Roda Jc,Fc chiasso etc.

Narudia hii cream ya hawa wachezaji ingechanganywa na Serengeti boyz wa Gabon hakika tanzania baada ya miaka kadhaa tungefika mbali sana.
 
Kikosi cha stars bila mkude ni utani aisee
Halafu mbona kila muda kikosi kinabadilika ?
 

Maelezo yako tu hapa yanaonyesha kuwa hujawahi kucheza Mpira halafu siyo Mtu wa Mpira hasa Kiufundi na ndiyo maana umeandika kwa kirefu hivi lakini unapopalenga ni padogo sana. Kuna mahala pia umenichekesha kama pia siyo kunisikitisha na kama kweli Tanzania tunao ' Mashabiki ' wa aina yako acha tu nafasi za 150+ katika Viwango vya FIFA.

Umemtaja hapo Mshambuliaji wa Kitanzania Rashid ' Chidi Boy ' Mandawa anayacheza mpira wa Kulipwa huko nchini Botswana kwa kwanini hakuitwa leo na Kocha Mayanga kwakuwa tu mechi yao dhidi ya Timu ya Township Rollers iliyocheza na Yanga alifunga magoli matatu peke yake ( yaani hat - trick )

Nani aliyekuambia kuwa Mchezaji anaitwa Timu ya Taifa eti kwakuwa tu amefunga katika mechi moja? Nina uhakika hata huyu Mchezaji Mandawa umemjua tu juzi juzi hapa baada ya Watangazaji akina Alex Luambano na Edgar Kibwana kufanya nae mahojiano ila huko nyuma kati ya Mimi na Wewe achilia mbali tu hata Kocha mwenyewe Mayanga hakuna aliyejua alipo.

Kiufundi tu kuna Vigezo vingi vya kumfanya Mchezaji fulani aitwe Timu ya Taifa kama vile kuwa Fiti kwa mechi, kutokuwa na majeruhi ya mara kwa mara, anapata nafasi ipi katika Kikosi je ni regular au ni irregular starter tu?, anaendana na mfumo halisi wa Mwalimu / Kocha wa Taifa?

Umeshajiuliza labda ni kwanini Beki wa Kitanzania Abdi Banda ' Binyo ' anayecheza mpira wa Kulipwa huko Afrika ya Kusini katika Klabu ya Baroka ameitwa katika Kikosi? Jibu ni rahisi tu kwamba Kwanza ni Mchezaji tegemeo katika hiyo Timu, pili anafanya vizuri mno, tatu muda mwingi yupo katika Kiwango na hapati majeraha mengi kama Mandawa wako huwa anayapata huko anakocheza nchini Botswana.

Umemtaja hapo Golikipa Deo Munishi ' Dida ' kwamba kwanini hakuitwa na nikapatwa na mshangao tena na ndiyo maana nasisitiza Kwako kwamba Wewe nahisi hata mpira wa Kiwango chochote hujawahi Kucheza na inawezekana hata Kushabikia mpira umeanza hivi karibuni ( na mpo wengi humu Jamvini ) na bado hamjakomaa katika kufanya ' Football Technical Analysis '.

Hivi unataka Kipa Deo Munishi ' Dida ' aitwe Taifa Stars kwakuwa tu nae anacheza nje ya nchi. Je unajua yuko nchi gani? Je huko aliko sasa anapata nafasi? Je Kiwango chake kimeimarika kiasi kwamba amemvutia Kocha Mkuu Mayanga? Je TFF na Wadau mbalimbali wa Mpira nchini wanamfuatilia kuweza kujua alipo na kiwango chake? Jibu hapa ni rahisi kama siyo jepesi la hapana na hata Yeye mwenyewe tu kama Mchezaji ameshindwa kuji ' brand ' kama ambavyo mwenzake Simon Happygod Msuva amekuwa akifanya mara kwa mara kiasi kwamba ameweza Kutushawishi Watu wengi tuanze Kumfuatilia na anafanya vyema kweli huko aliko nchini Morocco.

Unahitaji Kujifunza zaidi masuala ya Soka / Mpira ili siku zingine ukija humu uweze kutuaminisha kuwa umekomaa.
 
Maelezo mareefu yenye kujaa ukosoaji lakini pumba tupu!

Mleta mada kaelezea point mbili kubwa kumhusu Rashid Mandawa,,, kwamba ndiye mshambuliaji aliye katika kiwango bora hivi sasa ktk ligi kuu ya nchini Botswana kwani anayeongoza ufungaji magoli,
Pia akiwa ktk ubora wake ameweza kutupia hat trick dhidi ya Township Rolllers!!

Na mwisho mleta mada ameona udhaifu ni skouting ktk benchi la ufundi,,, kwamba pengine benchi la ufundi hawafatilii ipasavyo viwango vya wachezaji wetu mbalimbali waliopo ktk ligi za nje ya nchi yetu ndio selection ya wachezaji timu ya taifa inafanywa kimazoea!!!
 
Asante sana mkuu kwa ushauri wako. kwanza napenda kukupongeza sana kwa mada mbalimbali unazoziwasilisha humu. Labda nikukumbushe tu binadamu runatofautiana katika upeo wa kutoa au kuwasilisha mawazo yetu na pia ni haki kabisa mtu kutoa mawazo yake kikubwa tu asivunje sheria za nchi husika

Turudi kwenye mada, Pengine labda ungenishauri kuwa kile nilichokusudia kukiandika labda hakina mtiririko unao eleweka hivyo hoja yangu haina mashiko kuliko kuniattack kuwa sijacheza mpira na mengineyo.

Tuanzie kwa Rashid Mandawa, nilichoandika ni hivi Rashid ameifunga Township Rollers magoli matatu ili watanzania wenye upeo mdogo kama mimi wajue tunamzungumzia mchezaji wa aina gani.Sikuishia hapo nikaongeza kuwa Rashid amefunga magoli kumi na moja na zaidi. Cha kushangaza wewe mwenye upeo mkubwa wa soka hata hilo umeahindwa kulielewa na kukimbilia kuwa nimeanza kushabikia soka juzi.Mimi ni mgeni humu jamii forum hii ndio post yangu ya kwanza na najua watu kama nyinyi ukiambiwa nenda instagram uanze kufatilia habari za wachezaji wetu wanaocheza njee utasema instagram ni ya watu ambao sio educated. Je wewe ambae ni shabiki wa soka na umecheza mpira unawajua wachezaji gani wa Tanzania na idadi yao hadi sasa?

Deogratius Munish, una uhakika gani kuwa sina takwimu zake na wapi alipo?

Wachezaji wote wa Tanzania wanaocheza soka njee huwa na report habari zao kwenye page yangu ya Instagram @tanzania_pro_soccer_player hata huyo Rashid Mandawa nimeanza kureport habari zake nikishirikiana na killersportbotswana tokea amefika Botswana na mimi pekee ndio nafanya hivyo kwa wachezaji wetu wote wanaocheza njee na wengine ambao hata wewe uliecheza soka na uhakika hauwajui.
 
Kocha mwenyewe ameishajichokea cha muhimu amelazimisha kubalance na vusiwani kutoa lawama basi lakini sijaona jipya pale
 
Alifunga timu B ya Township Rollers wakati huo huo kikosi cha kwanza hakitishi kiivyo
 
Unamwita mchezaji kama Thomas Ulimwengu ambaye hata timu anayocheza sasa haijulikani na alikuwa majeruhi muda mrefu
 
mechi aliyofunga Rashid Mandawa goli tatu Town Rovers walipumzisha wachezaji wao wengi kwa ajili ya mechi na Yanga makocha wako sahihi kuwaita wachezaji wanaoona wanawafaa ndio maana timu ikivurunda wanatimuliwa kama mmewaamini waachieni wafanye kazi kwa uhuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…