Apitakujilamba
JF-Expert Member
- Sep 27, 2013
- 205
- 82
Tukirudi nyuma wakati wa Mwl Nyerere elimu ilikuwa sawa kwa watu wote nikimaanisha wa mjini au kijijini, tajiri au mtoto wa mkulima. Hali hii iliwezesha wale wanaopata fursa ya kuendelea mbele, kuendelea kwa kigezo cha ufaulu na nafasi zilizopo. Pamoja na uwepo wa shule binafsi lakini shule za serikali ziliendelea kuleta ushindani na kufanya vizuri iliyopelekea kuleta uwiano sawa katika elimu. Lakini hivi karibuni baada ya uanzishwaji wa shule za kata, shule za serikali zimeporomoka na kudhoofisha huo ushindani. Wakati huo huo kwa upande wa vyuoni kukiwa na changamoto ya bodi ya mikopo.
Nia ya kuanzisha bodi ya mikopo ilikuwa ni njema yaani kuwasaidia wanafunzi wengi kupata elimu ya juu. Na kigezo kikuu kilichotumika tangu mwanzo niufaulu wa mwanafunzi yaani daraja la kwanza mpaka la tatu kwa wanafunzi wanaochukua masomo ya sayansi na daraja la kwanza na la pili kwa wale wanaochukua mchepuo wa sayansi. Pamoja na kigezo cha ufaulu, pia kuna vigezo vingine ambavyo bodi wanatumia.
Kwa miaka ya hivi karibuni nimeona bodi kama wamepotoka kwa kuweka kigezo cha aina ya shule uliyosoma yaani serikali au binafsi kama ndio kigezo na baadae kufuatia ufaulu wa mwanafunzi. Kwa maana kuna wanafunzi wengi wanaoangukia kwenye daraja la kwanza na la pili kwenye shule za watu binafsi wakiwa wamekosa mkopo kabisa au wengine wachache wa sayansi wakipewa mkopo nusu kwa maana wajilipie ada yote ingali wanafunzi wengine waliosoma shule za serikali wakipewa mkopo asilimia mia ingali wakiwa wamepata daraja la tatu. Mimi huu nauona kama ni ubaghudhi uliodhahiri kabisa.
Pamoja watu wengi tutasema kwamba wanaosoma shule za serikali ni watoto wa wakulima, hi hali wale wanaosoma shule binafsi ni watoto wa matajiri, lakini kigezo hiki ni kigumu sana kukitumia kwa mfumo wetu wa taarifa. Kwa mfano kuna wazazi wengi wamejitoa mhanga kuwasomesha watoto wao shule binafsi kwa kutafuta mikopo mbali mbali kwa sababu labda mtoto alikosa shule ya serikali au sababu nyinginezo. Wengine wamesoma wa fedha za mifuko ya jamii ya baba zao ambao hawapo hai, wengine wamesomeshwa na ndugu baki tu ili mradi wamalize shule ya sekondari, kuna wengine wamesomesha watoto wao kipindi wanamalizia kazi zao na sasa ni wastaafu. Vile vile kuna watoto wengi ambao wamesoma shule za serikali wakati baba zao wana uwezo mkubwa tu, mfano enzi za ridhiwani alisoma Mkwawa sekondari wakati baba yake ana uwezo mkubwa.
Kwa kufanya hicho ndio kigezo cha kwanza kwa hakika itashusha morali ya wanafunzi wa shule binafsi kwa maana anajua apate daraja la kwanza au tatu bado hatajilipia tu. Pia inavunja moyo wazazi/walezi kwa kukazana kumpeleka mtoto shule binafsi ili afaulu ili apumzike swala la ada kwa mtoto wake. Wanafunzi wengi watataka kuingia shule za serikali kwa kujua anahitaji daraja la tatu apate mkopo wake, na hapo nafikiri serikali haijajiandaa kuwa na wanafunzi wengi kiasi hicho.
Kwa maoni yangu kigezo kikuu kibakie kile kile daraja la kwanza mpaka la pili wote wapate mkopo haijalishi ni kutoka serikalini au binafsi, halafu wale wa daraja la tatu ndio uingize kigezo cha shule za serikali na shule binafsi. Jambo kuu ni serikali inatakiwa kuziendeleza shule za serikali kufikia kiwango cha ushindani na shule binafsi.
Nawakilisha.