Ngaliwe
Senior Member
- Dec 30, 2015
- 164
- 374
Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa uhuru wa kujieleza kwa kila raia wake bila tashishwi ili mradi tu, uhuru huo hauingilii, kuvunja kutweza na kufanya dhalili haki ya watu wengine kutumia uhuru wao kama ulivyotolewa na katiba yetu.
Ibara hiyo inatanabahisha wazi kwamba: "Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati. Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii."
Neno msingi katika nukuu hii kwa muktadha wa makala haya ni maneno yaliyoyangulia kwenye ibara hii, "Bila kuathiri sheria za nchi". Haya yanabeba uzito mkubwa sana kwenye ibara hii, pamoja na kupewa uhuru wa kila mtu kutoa maoni yake kwa namna anayona inafaa, katika jamii iliyostaarabika Uhuru huo lazima pia uzingatie haki, heshima, hadhi na utu wa watu wengine.
Huo ndiyo msingi wa maelewano na tunu zetu adhimu katika Taifa letu, umoja mshikamano na amani, hizi zinashamiri na kustawi vema nchini kutokana na msingi huo, kwamba pamoja na kuwa tumepewa haki ya kutoa maoni, ni ukweli wa kiuumbaji kwamba kila mtu yuko tofauti sana na mwenzake, kwa maoni, mtazamo, imani na hata mwelekeo wa itikadi.
Ndiyo maana pamoja na tofauti zetu za makabila, imani,uwezo wa kiuchumi, mitazamo ya kisiasa bado tumeendelea kuwa Taifa lililoshikamana na kwa hilo tumekuwa watu wa kupigiwa mfano. Mwenendo wa Askofu Gwajima tangu amkashfu na kumtukana Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, umekuwa wa utata sana na mbaya zaidi amekuwa akitumia jukwaa la kanisa lake, ambalo bila shaka, lilisajiliwa kwa nia njema kwa ajili ya kuhubiri habari njema ya wokovu, lakini yeye akaligeuza kuwa kijiwe cha kusuta na kukashifu kila anayetofautiana naye mtazamo.
Kwa kuendelea kuchekewa bila kuchukuliwa hatua stahiki amekwenda mbali zaidi kiasi cha kujiona yeye ni mtu wa pekee sana nchini. Ni haki yake na waumini wake kutochanja chanjo ya Uviko - 19 kama wakichagua hivyo, ndiyo maana Serikali ilibainisha mapema kabisa kwamba, chanzo hizi ni hiyari, hakuna mamlaka inayomshuritisha mtu kuchanjwa, kwa kujua kuwa wapo walio na na mtazamo tofauti, waheshimiwe.
Kitendo cha Gwajima kujitokeza hadharani tena siyo mara moja kuwatuhumu viongozi kwamba wamehongwa ili walazimishe wananchi wachanjwe na eti wao viongozi wamepata chanjo ya ghiliba tu, ili washawishi raia wachamjwe, hakikupaswa kufika huku kilikofika. Tuhuma alizokuwa anatoa ukiondoa kwamba ni kejeli na dharau kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jambo ambalo ni kinyume cha Katiba yetu, lakini pia alikuwa anatumia mimbari ya kanisa lake, kinyume na usajili wa kanisa hilo.
Vyombo vilipaswa kuchukua hatua mapema, kwa sababu ujinai ulikiwa wazi, lakini wananchi tulibaki tunajiuliza hivi kuna watu walio na haki zaidi ya wenzao nchini kwetu, mtu anakejeli na kumfanya rais aonekane kama mtu anayewasaliti wananchi anaowaongoza lakini mamlaka zilikuwa kimya kana kwamba wao ni wageni waalikwa nchini. Ni kutokana na kukerwa na mambo hayo, ndiyo maana, wengi wetu tunapongeza hatua zilizochukuliwa na Bunge dhidi ya mbunge huyu, na mwenzake wa Ukonga Jerry Silaa.
Pongezi hizi si kwa sababu ya kupongezwa tu, zaidi sana ni kwasababu hatua hii ya Bunge imerejesha heshima na utu wetu kama Taifa. Waliokuwa wanatupeleka waheshimwa hawa ni kutufanya kuwa taifa la wendawazimu, ambalo kwalo kila jambo linaendeshwa hovyo hovyo, bila utaratibu.
Kwa hatua hii Bunge limeonyesha kwamba Tanzania ni Taifa linalojiheshimu linaloheshimu utu wa mtu na lenye heshima kwa viongozi wake
AHSANTE NDUGAI