Elections 2010 Kwa hili CCM au makampuni ya simu washitakiwe

Elections 2010 Kwa hili CCM au makampuni ya simu washitakiwe

Msharika

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Posts
947
Reaction score
70
Nimesikitishwa sana kwa kupata ujumbe wa kutoa ni moyo! Changia CCM kuanzia 300, 500 na 1000. Nimehuzunishwa kwani mimi si mwanachama wa CCM na wala sina ubia na chama hiki kilichojaa unyonyaji sana.

Nani kawapatia namba yangu? Kama ni mashirika ya simu kwanini yanatoa namba za wateja wake bila hidhini ya mteja? Ningeomba ufafanuzi katika hili na hatua stahili. Huu ni usumbufu kwa wasiousika
 
Kiongozi,

Nini hasa kimekukera? Ujumbe kutoka kwa provider wako?

Sioni sababu ya wewe kuwa na hasira na provider wako. Huo ni mfumo wa kawaida wa matangazo ambao taasisi wanautumia kufikisha ujumbe kwa urahisi na kwa haraka kabisa kwa wananchi. Nafikiri hilo sio tangazo la kwanza kukupata. Kama ni mteja wa tigo simba sports club walitumia mfumo huo huo kuwajulisha wananchi waichangie. Wananchi wote waliokuwa wateja wa tigo haijalishi ni wanachama au wapenzi wa simba waliupata ujumbe.

Kwa hiyo hilo sio kosa la CCM na wala sio kosa la provider wako wa simu. Labda liwe kosa kwa sababu tu hamkuwekeana mkataba wa matumizi ya namba yako ya simu na usiri wake.

Angalia hata kwenye barua pepe. Mtu anatokea huko anakutumia mail hata humjui.

Ndivyo makampuni yafanyavyo. It is a business to them. Mara nyingi watu huwa hatuangalii SLA za products nyingi.

Ila usichukie kuchangia chama chochote kama unatamani kukichangia. Hiyo ni sadaka bwana msharika
 
Shagihilu wasamehe hawatarudia. Kunywa taska 2 lete risiti nitakurudishia
 
Heshima kwako Mshirika, Hata mimi nimepata ujumbe kama wako,kwa kweli nilikereka kupita maelezo. Hivi hawa CCM wanafikiri hatujui jinsi walivyotutumbukiza kwenye lindi la umasikini bila sababu za msingi.Bila aibu wanatuomba fedha zetu kiduchu tuwachangie wakati tunajua wanazo njia za mkato za kupata fedha za kuwanunulia wapiga kura kapelo,tshart,kanga na nyama za nyumbu.
 
hakuna anayesema kuchangisha ni mbaya, lakini wanamchangisha nani ndo hoja hapa. wengine si washabiki wala wanachama wao sasa ya nini kutukera na kutusumbua na sms tena sio mara moja basi, mara kadhaa......

Inaudhi sana tena sana, hasa pale ninapofikiri ccm na uchafu wa viongozi wake, yaani ndo nasikia hasira kabisa
wish they had a different arrangement kwa kweli
 
hakuna anayesema kuchangisha ni mbaya, lakini wanamchangisha nani ndo hoja hapa. Wengine si washabiki wala wanachama wao sasa ya nini kutukera na kutusumbua na sms tena sio mara moja basi, mara kadhaa......

Inaudhi sana tena sana, hasa pale ninapofikiri ccm na uchafu wa viongozi wake, yaani ndo nasikia hasira kabisa
wish they had a different arrangement kwa kweli


mimi sijapa huo ujumbe but i guess walio pata ni wale wanaotumia mtandao wa ra mwenye share kubwa fisadi
 
mimi sijapa huo ujumbe but i guess walio pata ni wale wanaotumia mtandao wa ra mwenye share kubwa fisadi

dah zain wanatuma sana mkuu, mpaka unakereka, natamani ningeweza kuwarudishia majibu kwa ile namba wanayotumia.........
 
Wajumbe tusianze ubaguzi isije ikafika wakati mkashindwa ata kuongea na mtu kwa sababu ya chama chake unajua kupewa taharifa ni jambo la msingi lakini si lazima taharifa hizo zikupendeze , kwa mfano ungetumiwa ujumbe wa kwamba umeshinda zawadi usingewauliza kwanini wametumia namba yako pasipo ruhusa yako
wajumbe naomba umoja kwa taifa uendelee watu wachache kupiga pesa usifanye tuchukiane wavujajasho
 
Nilijua tu CCM kwa kujipendekeza lazima waanze kusumbua watu na sms zao za kijinga.
 
Nimekerwa na ujumbe mfupi wa maandishi kuingia kwenye simu zangu kutoka CCM kama vile makampuni ya simu yanavyotutumia 'promotions' na 'updates' zao. Mimi si mwanachama wa CCM sasa najiuliza inakuwaje?
Ujumbe niliopata kutoka CCM kupitia Zain nanukuu kama ifuatavyo: “Kutoa ni Moyo! Unaweza kuchangia CCM kwa kutuma neno …” . Pia nimepata ujumbe huo kupitia VodaCom Tanzania wakiwatumia watu wanajiita PUSH MOBILE. Ujumbe mwingine kupitia Zain unaomba nichangie kupitia CRDB bank na akaunti imewekwa. Nilijaribu ku’forward sms za CCM kupitia Zain hazikubali kwenda!
Nijuwavyo mimi taarifa ikiwemo namba ya mteja wa simu haitolewi bila ridhaa ya mteja kwa mtu mwingine. Na inatumika na kampuni ya simu kwa ajili ya mambo yahusuyo kampuni hiyo; sasa CCM imepataje namba yangu? Na inanileteaje ujumbe unaonikera? Je Zain na Voda wanafaidika vipi?
Nahisi CCM haiwezi kupata bil. 40 zote kutoka kwa wanachama wao kupitia simu hivyo wanaingiza na wasio wanachama kwa kigezo kisichojulikana ili kuhalilisha mifedha waliokwisha kwapua!
Njia wanayotumia kutoa maelekezo ya kuchangia kupitia vyombo vya habari kama kwenye The Citizen, pp. 17 ni sawa lakini sio kuniletea kwenye simu zangu.
Nilikwenda kulalamika VodaCom wakaniambia hiyo sms unapata baada ya ku’subscribe’ lakini mimi sikufanya hivyo. Leo nitaelekea Zain.
Kwa ICTs kifuatacho kinawezekana: mara sms ya CCM inapoingia kwenye simu yako, kiasi Fulani cha pesa kinachukuliwa, kwani VodaCom walionyesha kuwa mara upatapo ujumbe kutoka PUSH MOBILE (wanawalipa Voda kwa kutumia namba za wateja wao) kiasi cha pesa kinakatwa. Na wasiwasi haya makampuni ya simu yanayotumiwa na CCM kama yatalipa kodi kipindi hiki cha uchaguzi hasa yanayotuma ‘unsolicited sms from CCM’!

Bright.
 
Kama Zain au Voda watakuwa wamekata baadhi ya pesa kwenye simu yako bila ridhaa yako kama kweli huja subscribe ushauri nenda Zain na Voda waombe wakutolee copy ya matumizi yako halafu wasiliana na mwanasheria atakusaidia na hilo litasaidia wengi wanaoibiwa bila kufahamu.
 
Pole. Wengi tusio wanachama wa CCM tumepata ujumbe huo na nadhani wale watakaofanya makosa ya kujibu kwa kutumia namba zilizotolewa watakuwa wameliwa fedha zao kwa kufanya hivyo! Wakati mwingine ni aibu kwa chama kikubwa kama CCM chenye matajiri wanaojipendekeza left and right kinashindwa kupata hizo fedha na badala yake wanawasumbua wananchi maskini wasio na mbele wala nyuma. Ni unyama wa aina fulani!
 
Tafadhali tiGo sihitaji hizi meseji zenu za kijinga " tuma meseji kuchangia CCM kwa shilingi 300,500 ama 1000! wakubwa tuheshiame! Chama la kifisadi bado mnataka kutuibia hata tusipopataka? Tafadhili jamani nitachukia niache kutumia Mobile eboooooooooooooooooooo
 
Pole. Wengi tusio wanachama wa CCM tumepata ujumbe huo na nadhani wale watakaofanya makosa ya kujibu kwa kutumia namba zilizotolewa watakuwa wameliwa fedha zao kwa kufanya hivyo! Wakati mwingine ni aibu kwa chama kikubwa kama CCM chenye matajiri wanaojipendekeza left and right kinashindwa kupata hizo fedha na badala yake wanawasumbua wananchi maskini wasio na mbele wala nyumba. Ni unyama wa aina fulani!
Nimepapenda kwenye red ni typing error au ndicho ulichokusudia.
 
Hiki ni kiini macho cha CCM magari walishaagiza hela walipata wapi leo wanakuja na michango huo ni uongo hela walishachota wanachofanya ni kuzuga watu na vyama vya Upinzani
 
Nijuwavyo mimi taarifa ikiwemo namba ya mteja wa simu haitolewi bila ridhaa ya mteja kwa mtu mwingine. Na inatumika na kampuni ya simu kwa ajili ya mambo yahusuyo kampuni hiyo; sasa CCM imepataje namba yangu? Na inanileteaje ujumbe unaonikera? Je Zain na Voda wanafaidika vipi? [/FONT]
Nahisi CCM haiwezi kupata bil. 40 zote kutoka kwa wanachama wao kupitia simu hivyo wanaingiza na wasio wanachama kwa kigezo kisichojulikana ili kuhalilisha mifedha waliokwisha kwapua!
Njia wanayotumia kutoa maelekezo ya kuchangia kupitia vyombo vya habari kama kwenye The Citizen, pp. 17 ni sawa lakini sio kuniletea kwenye simu zangu.
Nilikwenda kulalamika VodaCom wakaniambia hiyo sms unapata baada ya ku’subscribe’ lakini mimi sikufanya hivyo.


USISHANGAE kama wewe ni mwanaCCM kweli. CCM walifanya mchezo huu wakati wa uandikishaji kura wa pili kwa kupitia kwa wajumbe wa shina (Nyumba kumi). Wajumbe hao walipewa form maalum kupita kwenye kaya zao kandikisha majina ya wapiga kura na kuwaomba pia namba za simu za mkononi. Lakini wakazi hawakuelezwa ni za nini. Kwa wale waliokuwa macho waliwauliza wajumbe hao kadi zao za kupiga kuar zinauhusianao gani na CCM. Binafsi niligundua hilo baada ya kuona fomu hiyo ina nembo ya CCM na si ya serikali au Tume ya uchaguzi.
Hivyo usirukie mambo bila kujua, ma Carl Pieters wapo huko mitaani wakitafuta data zenu!!!
Kuhusu kukatwa hizo fedha inawezekana kabisa, makampuni ya simu yatakata gharama za ujumbe wako. Hii ni njia mpya kuchangisha pesa kutoka kwa wadau. Redio Tumaini, ya Wakatoliki, wame/natumia njia hii kuchangisha pesa za kuiwezesha matangazo yake yawe kwenye satelaiti. Kikuu sasa kuhusu matumizi ya njia hii ni kuwepo kwa regulating and auditing bodies ilikuhakikisha kwanza kodi stahiki inalipwa TRA na haziendi kwenye matumizi mabaya. Ni vyema vyama vingine pia vikatumia njia hii ili kujidhatiti kimapato toka kwa wanachama wao wadogo wadogo ili wachangie gharama.
 
namba hawajapewa na kampuni za simu wala nini .............ccm mafia wewe!
 
Back
Top Bottom