hakuna anayesema kuchangisha ni mbaya, lakini wanamchangisha nani ndo hoja hapa. Wengine si washabiki wala wanachama wao sasa ya nini kutukera na kutusumbua na sms tena sio mara moja basi, mara kadhaa......
Inaudhi sana tena sana, hasa pale ninapofikiri ccm na uchafu wa viongozi wake, yaani ndo nasikia hasira kabisa
wish they had a different arrangement kwa kweli
mimi sijapa huo ujumbe but i guess walio pata ni wale wanaotumia mtandao wa ra mwenye share kubwa fisadi
Nimepapenda kwenye red ni typing error au ndicho ulichokusudia.Pole. Wengi tusio wanachama wa CCM tumepata ujumbe huo na nadhani wale watakaofanya makosa ya kujibu kwa kutumia namba zilizotolewa watakuwa wameliwa fedha zao kwa kufanya hivyo! Wakati mwingine ni aibu kwa chama kikubwa kama CCM chenye matajiri wanaojipendekeza left and right kinashindwa kupata hizo fedha na badala yake wanawasumbua wananchi maskini wasio na mbele wala nyumba. Ni unyama wa aina fulani!
Nimepapenda kwenye red ni typing error au ndicho ulichokusudia.
Mnajipa pressure bure, kama hamtaki kuchangia, bonyeza delete.
Nijuwavyo mimi taarifa ikiwemo namba ya mteja wa simu haitolewi bila ridhaa ya mteja kwa mtu mwingine. Na inatumika na kampuni ya simu kwa ajili ya mambo yahusuyo kampuni hiyo; sasa CCM imepataje namba yangu? Na inanileteaje ujumbe unaonikera? Je Zain na Voda wanafaidika vipi? [/FONT]
Nahisi CCM haiwezi kupata bil. 40 zote kutoka kwa wanachama wao kupitia simu hivyo wanaingiza na wasio wanachama kwa kigezo kisichojulikana ili kuhalilisha mifedha waliokwisha kwapua!
Njia wanayotumia kutoa maelekezo ya kuchangia kupitia vyombo vya habari kama kwenye The Citizen, pp. 17 ni sawa lakini sio kuniletea kwenye simu zangu.
Nilikwenda kulalamika VodaCom wakaniambia hiyo sms unapata baada ya kusubscribe lakini mimi sikufanya hivyo.