activisty
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 315
- 107
KWA HILI CCM MMEZIDI ITS A SHAME
Ni jambo la ajabu kuona watu tena viongozi wakituaminisha UONGO WA WAZI WAZI.Ni jambo la ajabu sana kuona mjumbe wa bunge maalumu akiunga mkono ukiukaji wa haki za msingi za raia ndani ya jamhuri ya Tanzania huku mjumbe huyo tukimtegemea kutuandalia katiba mpya na ya haki.Haiwezekani ni aibu kabisa, kwani ninapotazama bunge la katiba kama mtanzania wa kawaida ninaelewa na naweza kuchambua hoja kiusahihi kabisa na kutambua lipi lawafaa na wanalolihitaji watanzania wanyonge na lipi ambalo hawalihiitaji kabisa.
Hoja ya wananchi kupata habari ipo wazi kabisa. Hata kama habari hiyo haiko sahihi bado raia ana haki ya kuipata na kuichambua ilimradi habari hiyo ina umuhimu na umaalumu kwani inagusa sehemu ya maisha yake na jamii kwa ujumla.Sasa ntakushangaa wewe mjumbe maalumu wa bunge la katiba ukipiga makofi na kushangilia ati kwa kuwa hoja NAFKI, inayoungwa mkono na wanachama wa chama chako kwa sababu tu, ati imetolewa na mjumbe wenu (ccm) basi unaikubali.
Haiwezekani kuwa wajumbe wa ccm, wanashangilia hoja ya chawenye ati waandishi wa habari wasiruhusiwe katika vikao vya kamati, kwani ndani ya vikao hivyo mengi hujitokeza, na ati habari itolewe na mwenyekiti au mjumbe atakayeruhusiwa na mwenyekiti wa kamati husika kwa raia yaani ikiwa na maana kwamba habari tutakazozipata ni zile tu, zitakazoonekana na mwenyekiti wa kamati kuwa ndizo watanzania tupewe, au tusipewe, nay ale yaliyojadiliwa ndani ya kamati hizo hatuna haki ya kufahamu kwani hakuna waandishi wa habari hakuna camera hakuna haki kwa waandishi wa habari kupata na kutoa habari kwa umma yaani raia hatupaswi hatuna haki ya kufahamu au kupata taarifa za process nzima yauandaaji wa katiba iyo mpya
Bila wasiwasi CCM wawakilishi wao wanapigia makofi unyimwaji wa haki ya kupata habari kuhusiana na suala nyeti ndani ya vikao vya kamati vya bunge. Cant you see? Its enough!!Mmeshatudanganya vya kutosha hili liko wazi. Wakina Halima,oliechi,machari, wametoa hoja sahihi kabisa na iko wazi ya nini mnasita kuhusu hilo?demokrasia iko wapi?wasomi mko wapi?BADILIKENI leteni hoja za msingi na msiwe na mawazo kuwa eti kwa kuwa rasimu mtakayoiandaa italetwa kwa wananchi ili tuipigie kura ya kuikubali au kuikataa kama katiba mpya basi ndo mpitishe hoja nafki kama hizo, je! Amuoni aibu kwa posho nyingi mnzolipwa?mnamuwakilisha nani?ni raia yupi mwenye akili timamu atakubaliana na hoja za kudhalilisha kama hizo?walemavu mnawaandamiza ndani umoumo, vp hawa huku mitaani?na raia je?
Acheni kufanya kazi za kimazingaombwe.Katiba ni jambo muhimu na si la mchezomchezo tu,mnatuzunguka kwenye kura ya siri na wazi je haitoshi?Mimi nasema ni bora wanaoonekana kushindwa kazi hapa mwanzoni wakaondolewa kabisa au bunge hilo lifutwe kabla ya kufika uko mbele huku tukipata hasara kubwa.wana ccm kwa hili mmezidi ni aibu ya wazi its enough.Kwani ni;
bora mtu mwenye uwezo wa kufanya jambo pasipo kufikiri lakini kwa usahihi kabisa, kuliko mtu Yule anaefanya jambo lilelile kwa kufikiri lakini pasipo na usahihi wowote