Kwa hili,Clouds fm mtajutia

holygrail

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2012
Posts
1,303
Reaction score
597
Uamuzi wa kuwasimamisha b12,Adam Mchomvu na Diva sio wa busara kibiashara.

Kipindi cha xxl kimekuwa na wapenzi wengi sana kutokana na chemistry nzuri ya mchomvu na b12. Hawa jamaa wanajua sana na ndio maana kipnd chao kina wadhamini wengi sana.

Namshauri Ruge asikurupuke akawafukuza hawa vijana kwani atarudisha nyuma clouds fm kimapato.
 
au wadau mnasemaje
Power Breakfast chini ya Kipanya,Fina na Hando ndo kipindi kilichokua kikiingiza pesa nyingi kuliko vipindi vyote na walikua na umaarufu mkubwa, lakini walipoenda kinyume na utaratibu walifukuzwa kazi(Fina na Kipanya) na radio ipo hadi leo na bado P/breakfast inakimbiza kwa mapato,so wasijisahau ile ni radio ya Kusaga siyo yao.
 
clouds ni maarufu zaid ya hao mzee,kama wao waliweza wengine hawatashindwa, swala la muda tuu
 
acha kukariri.... Nani aliamini KASEJA angeondoka simba...?
 
Kumbe bado Clouds inapendwa sana hapa J.f.....NAFURAHI kwa Hilo.
 
Unampangia Boss Ruge wakati anaanzishaa ulikuwepoo
 

Una hangaika bure tuu, clouds wamepanga hii kitu kutafuta attention. Jaribu kufanya kauchunguzi,hakuna aliyefukuzwa hapo wala kusimamishwa.

Wanajaribu kutafuta attention.
 
Pengine hamjui Maestro Ibrahim Masoud ni moja ya vichwa pale mawingu na kuchomoka kwake si jambo dogo.Maestro alikuwa mzuri zaidi kama director na mbunifu wa vipindi vingi.

Lakini pamoja na mapungufu yake yoooooote! Ruge ndio Ingine ya Clouds na ndio kila kitu hasa upande wa ubunifu na kuvumbua vipaji na namna ya kuvitumia.Hakuna mtangazaji ambaye kuondoka kwake kutaitikisa Clouds.

Ile dream team ya akina ML Criss,Bonny Love,Bobby,Fina,Amina Chifupa,Masoud Kipanya,Seven,Jimmy Kabwe,DJ Charles,DJ Boogie Master,Gadner Habash,Othman Njaidi etc woooooote hawa hawapo tena na walikuwa vichwa kupitiliza lakini bado radio haifanyi vibaya kama tulivyofikiri ingeweza kufa kabisa.

Kuna aliyetarajia kipindi kama cha Aspen kile cha Taji Liundi kuna mtu angeweza kufanya kiendelee kuwa juu? Lakini Sebastian Ndege akaja na njia panda na kinafanya vizuri ingawa si kama zamani kutokana na pia mabadiliko ya mambo mengi kama kuongezeka kwa matumizi ya vitu vingine kama TV programmes, watu kushinda wakichat kwenye mitandao n.k

Nadhani Ruge akitoka pale ndio Mawingu inaweza kwenda chini lakini si hawa watangazaji.
 

..,,, MTAZAMO wako una make sense.
 
Last edited by a moderator:
mh! Lakini kweli. Nimegundua hii ki2 ni stunts tu.
 
kuchukia chombo cha habari ni upunguani...labda ukate maskio...uzibe kabisa.

ukweli naikubali cloud fm hasa kwenye kipindi chao cha magazeti. Sijui ndio wanakiitaje? Huwa jamaa wanakuwa kama watatu hivi mmoja anasoma wengine wana toa komenti. Safi sana kwa kweli.
 
Amakweli jahazi sijawahi kuona! Naipenda cloudz na vipindi vyake! Wako vizuri wanasherehesha!!
 
Clouds ni taasis so mmoja au wawili na hata wakitoka mfumo wa kitaasisi utaibeba
 
Ruge ni creator,mfano kwenye soka kuna watu kama Arsene Wenger & Jürgen Klopp,hawa watu ni mabingwa wa kunyanyua vipaji ambavyo dunia ilikuwa haivipi nafasi na kuvifanya kuwa na World Class Quality.Hata ukiwatolea watu waliokwisha kuwa mastaa still watatengeneza mastaa wapya.Na Ruge yuko hivo,so namuunga mkono jamaa hapo juu aliyesema akitoka Ruge ndo Cloudz itatetereka
 
wewe uliyeandika hii thread ni b12 au Adam Mchomvu au Diva? au umetumwa na hao? kwendraaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…