Mkuu Mwanakijiji heshima kwako.
Nakubali ulichokisema kipo lakini sio kwa asilimia mia moja zote.
Mkuu wewe umeongea kama mwanaume anayewajua wanawake lkn mim naongea kama mwanamke ambaye ndiye ninayetongozwa.
Sio kweli kuwa wanawake wote tunatongozwa baada ya kuvutiwa na wanaume kisha kujilengesha kwao ili watutongoze.
Mim kama binti,nina uzoefu wa kutongozwa tokea niko shule,mim na rafiki zangu mara nyingi tu ilikua inatokea tunatongozwa na vijana ambao kamwe hatukuvutiwa nao na hivyo tuliwakataa.Tena unakuta wengine unajikuta unajenga kama kachuki au kahasira fulani juu yao sababu kila ukiwaambia haiwezekani tukawa pamoja wao wanazidi kukufuatilia,mara leo card mara kesho kampa mtu pesa akuletee,mara sijui kesho kafanya hivi jambo ambalo linageuka kero.
Sio kweli kwamba wanaume wote tulionao sisi ndio tumewachagua,asilimia kubwa wanaume ndio wanavutiwa na sisi kisha wanatuona bora kuliko wengine machoni mwao kutokana na muonekano wetu au kutokana na tabia zetu kuwavutia hivyo wanatuchagua na kututongoza.
Swali langu kwako mkuu ni kwamba,kama kweli sisi wanawake tunatongozwa baada ya kuwa tumevutiwa na wanaume na kuwajengea mazingira ya kututongoza KWANINI WAPO WANAUME WANAOTONGOZA NA KUKATALIWA?
Tena saa nyingine unakuta kuna mwanaume amezoea anakubaliwa na kila mwanamke anayemtongoza lkn ipo siku inatokea anatongoza msichana lakini huyo msichana anamkataa huyo kaka mwenye maujuzi yote ya kutongoza.