Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
-
- #41
Tunaamini kuwa mwanamke anahitaji kuwa na 'hisia' na mtu kumbe wapo wanawake ambao nao tendo hilo ni kama mazoezi ya viungo tu au kama kashata! wanakula wakiwa na hamu na wakimaliza hata hawakumbuki!
....mmmmh....NSA and one night stand...just saying!
Kaazi kweli kweli! Yaani hata soga tu nazo ziwe zinajadiliwa kwa kutumia sijui ma sample space na ma nini nini? Mweh!
unajua umefanya wazee wengi hapa wanyong'onyee ghafla!?
Mambo ya usawa siku hizi, kama nyie mnacheat kwa nini sie tuendelee kufa kwa pressure? Uzuri wetu tunafanya mambo kwa akili sio kama nyie mkishaogeshewa maji ya karafuu basi yale ya hiriki hamkumbuki tena. Chezeya wanawake weye!
msinyong'onyee....huo ndio ukweli.....
upo bi dada?msinyong'onyee....huo ndio ukweli.....
Unachofikiri ni soga si soga, unafikiri tu kwamba ni soga.
Duuuh..roho imeniumaaaaa!
Tulikuwa kwenye kikao kidogo cha wazee kijijini na tukawa tunazungumza mambo mengi. Kama kawaida mambo ya watu kucheat yakajitokeza mara moja kwanza ilikuwa hoja ya "kina nani wanacheat zaidi kati ya wanaume na wanawake". Jibu la kwanza ambalo lilionekana kwa urahisi - bila watu kufikiria sana na lilitoka kwa wanaume tena kwa fahari - ni kuwa wanaume ndio wanacheat sana. Hasa ni kwa sababu kubwa mbili mara nyingi (kama siyo zote) wanaume ndio hutongoza zaidi na pili wanaume wanaonekana wanakodolea macho ""kila chenye sketi kipitacho kikitingishikika". Wakati wanaume wanaendelea kujisifu kauli zetu zilijikuta zinakatishwa na moto wetu kupoozwa kama chuma cha moto kinapotumbukizwa kwenye maji!
"Mnajidanganya tu" alisema dada mmoja kwa sauti ya utulivu huku akiendelea kula kuku wake wa kuchoma. Macho yetu yalimgeukia kwa ghafla na mara moja tukapoteza kujiamini; wanawake wenzie pale kikaoni walimuangalia kwa macho yaliyojaa kila alama ya umbea (mshangao, dukuduku, shuku, kebehi... n.k).
"Tunajidanganya?" mmoja wa wazee pale kikaoni (I swear it wasn't MOI)
Well, dada yule alianza kutuelezea kwa sauti iliyochagua neno moja moja utadhani mashine ya kupigia chapa. Lakini kimsingi alisema mambo yafuatayo ambapo alipomaliza na kurudia kisusunilo kilichobakia mezani baadhi yetu tulitafuta gia za kutokea kikaoni! Alisema kwamba:
a. Wanaume wanadanganywa kirahisi kitandani! - mwanamke anaweza kupiga kelele na kusema maneno yote matamu kiasi cha kumfanya mwanamme afikiri kuwa ndiye aliyebuni na kukiunda kitendo hicho. Mwanamme anavyoitikiwa wakati wa shughuli inamjenga mno "confidence" yake kiasi kwamba hawezi kuamini kabis akuwa mwanamke wake anaweza hata kutoka nje - ambako nako anaweka mbwembwe zilizojaa iliki, mdalasini, limau, pilipili mbuzi, pilipili hoho, karafuu na thyme! Kelele za kitandani zinawapumbaza wanaume na mwanamke mjanda hujua kelele zipi za kuziingiza siku ya kwenda kucheat!
b. Wanaume wanafikiria wanawake wote wanahitaji hisia kufanya tendo: Kuna imani kuwa mwanamke hawezi kwenda na kufanya tendo hilo na mtu yeyote bila kuingiza hisia ndani yake. Yaani, wanaume wanafikiria (tunafikiria) kuwa ni sisi tu tunaoweza kwenda kulala na mwanamke na kesho yake kumfikiria mwingine. Matokeo yake wazo la kwamba mwanamke kwa vile anaonesha anakupenda sana na anakufanyia mambo mengi anapata pia pembeni na labda zaidi ya mtu mmoja haiingii akilini. Tunaamini kuwa mwanamke anahitaji kuwa na 'hisia' na mtu kumbe wapo wanawake ambao nao tendo hilo ni kama mazoezi ya viungo tu au kama kashata! wanakula wakiwa na hamu na wakimaliza hata hawakumbuki!
Yule dada alisema kitu cha kushangaza kuwa wapo wanawake hata hawakumbuki kabisa wanaume waliolala nao; na wengine ndio wale wanaoweza kwenda mahali - hasa kwenye visafari vya kikazi - akajipatia mwanamme wa usiku mmoja (one night stand) na wala asihangaike naye tena wala kutaka kujua alimradi alitumia kinga!
Baada ya kujaribu kubadilisha mazungumzo wazee wazima tuliondoka tukiwa na mawazo sana....
Kwa ufupi.. dada zetu nyie wajanja a.k.a mashapu!!! sijui ni vizuri au vibaya!!