Kwa hili Gazeti la Mwanahalisi liwaombe radhi Watanzania

Kubenea yuko sawa tu. Yaani hapo wote wachafu. Kuanzia Muhando na wenzie mpaka Waziri na wenzie. Wote kwa wakati wao na mahala pao ni wachafu. Hakuna anayechafuliwa hapo.
 

Maovu ya Mhando na watendaji wa TANESCO hayajaanza leo kuanikwa hadharani...!! Uzuri ni kwamba, katika kashfa hii ya TANESCO wamehusishwa hadi wanasiasa ambao wana majukwaa ya kuzungumza pasipo kumwogopa yeyote! Katibu Mkuu Maswi amewachana TANESCO hadharani pasipo kuumauuma maneno!! Jana, Profesa Muhongo nae amewachana hadharani pasipo kuuma uma maneno!! Sasa basi, hao ni wakati wa hao watuhumiwa kujitokeza na kuyasema mabaya ya Maswi hadharani badala ya kupita kulialia kwenye magazeti ambayo; kimsingi hakuna gazeti hata moja TZ lililo huru!! Pamoja na kudai kwamba Maswi ameteka mkataba wa tenda na kuupeleka kwa Puma Energy lakini hajatokea yeyote anayesema Maswi amelipwa shilingi ngapi zaidi tu ya kulalamika kwamba amekiuka sheria! Kama kukiuka sheria kunaweza kuokoa fedha za Watanzania basi kwangu inaweza kuwa ni heri zaidi kuliko kufuata sheria ambazo zinawanyonya Watanzania! Ukiangalia vizuri habari hiyo ya Mwanahalisi utaona wazi kwamba walichotaka kufanya ni ku-dissolve yale yanasemwa dhidi ya Mhando! Hata hivyo, ukiisoma kwa makini utakuta jinsi ambavyo confidence ya Mwanahalisi haipo kabisa kwenye habari hiyo! Kilichofanywa na kambi ya Mhando ni kwamba, baada ya kuona Raia Mwema wametoka na habari inayoeleza ufisadi wa vigogo wa TANESCO, ndipo nao wakaamua kutafuta gazeti ambalo linaaminika kidogo!!! Hakika hapa, ni ama Mwanahalsi wametumika au hawakufanya utafiti wa kutosha!!
 
ritz kashomeshwa ccm kivukoni haoni wala hasikii ni kansa ya ubongo ukishaipenda ccm maana ni sawa na dini ya mashetani hawajui kama kuna mungu wala ubinadamu

Hahaaaaa ritz kasomeshwa chuo cha mwalimu nyerere(ccm kivukoni enzi hizo) lol
 


Nani anayo cv ya kubenea jamani,atuwekee hapa
 
Hili gazeti ni bingwa la kuandika udaku na majungu siku zote uwa naliweka kundi moja na KIU, UWAZI. leo baada ya bajeti kusomwa limeabika kwa majungu.

Ukweli daima unauma hususani kwa wale wasiopenda kuambiwa ukweli mngekuwa na uwezo wakuyafuta mngeanza na mwanahalisi,raia mwema na tanzania daima jambo leo lina damu yenu.Uzuri wa wananchi wa leo wanauwezo wa kumbembua pumba na mchele. Ritz zile enzi za Always boss is right zilishapitwa na wakati.Hizo bil 3 ambazo unasema Maswi ameokoa ni sawa ila mgao wake utakapo wekwa hadharani utashangaa.Baada ya Mhando kuanikwa the next ni Maswi ni mengi hatuyajui wait n see
 

kwa hili kaka tupo pamoja
mafisadi ni lazima wakemewe,tusiwape nafasi kabisa,kama wameweza kuwarubuni wabunge ili wampige chini waziri na katibu wake,je watashindwa kuwanunuwa akina mwanahalisi?
 
Ingawa ni habari za kumtetea mhando! Hakika hizi habari si za uwongo ni za kweli kabisa. hii imetokana na sheria zete kuwalinda wafanyakazi hata kama wanafanya wizi au uzembe. Kwa alichofanya Maswi ni kama vile uku mitaani ukikamata mwizi choma moto ingawa sheria haziruhusu. hivyo Maswi kamchoma moto Mhando kwa ubadhirifu ingawa sheria zinambana. Swali la kuwauliza mwanahalisi ukiona mtu anahujumu uchumi makusudi utamwacha eti sheria inamlinda? Hongera Maswi maana huyu Daffi ndiye angekukaanga baadaye kama ungeacha uchafu huu utendeke!
 

Pesa pesa sabuni ya roho. ukiona hivyo ujue kuna mtu alinunua siku ile ili kufunika kombe mwanaharamu apite. lakini Mungu ni mwema
 
Mwanahalisi ni gazeti bora kuliko yote Tanzania,tungekuwa na magazeti matatu tu ya aina hii maendeleo yangepatikana. Linafanya mambo yake kwa utafiti mkubwa,ona hata Usalama wa taifa umeshindwa kujibu kwa ufasaha no. za simu kama ni za watumishi wao au laa. Kwa hili naona hawana haja ya kuwaomba Watanzania radhi kwani wana uhakika na walichoandika.
 
Mkuu sema ana mapenzi na magazeti hayo. Mahaba yanajumuisha kurembua pamoja na mambo mengine.
 
Jamani unajua hakuna mtu wa kumwani asilimia mia hapo> Usie ukashangaa baadaye kugundua kwamba pia kulikuwa na mizengwe kuipatia puma deal vilevile. Mimi hizi habari bado nazichukulia kwa tahadhari. Sija'side' na upande wowote bado. Lazima kuna a 'dead fish' somewhere!



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…