Innocizy
JF-Expert Member
- Dec 5, 2011
- 1,736
- 1,056
Naomba niweke wazi kwanza kwamba mm si shabiki wake hata nusu. Lakini ni miongoni wa watu wanaotumia muda mwingi ktk social media ambako siku hizi hata TV na redios hazioni ndani kwa social media.
Mapema mwezi huu(sina hakika sana) zilisambaa picha za kijana Ommy Dimpoz akiwa kavaa "kishamba" ktk treni kana kwamba ni "m-bara" anaingia pale stesheni(kwa wale wa zamani mwakumbuka kelele za walete walete wa bara haooo,pale stesheni)
Picha hizo zilizua sana mjadala ktk hizi social networks za hapa kwetu na mijadala mingi ikiwa ni kumponda huyu kijana kwamba alikuja na furushi akiwa mshamba hajui kitu, na kwamba sahivi "anaringa" na anajisikia kwa kuwa kapata "vihela" lakini ajue yeye bado "wakuja" tu.
Sasa kijana akaamua kutoa picha akiwa na Vanessa Mdee na wamebeba lile lile furushi ikiwa ni project yao mpya inayokuja hivi karibuni. Kijana akaenda mbali akitusihi watanzania tuache "kukurupukia" mambo na kupashana habari ambazo sio za kweli.
Hapo ndio kanigusa.
Sisi watanzania tumekuwa watu wa "kunata" na beat iwe reggae hip hop mduara au blues sisi tumo tuu.
Nampongeza sana kijana kwa kuliona hilo na kututega tena na kiukweli ametuteka wengi sana maana ni wengi sana waliamini zile picha ni za kipindi anakuja kweli Dar.
Pia katukumbusha kwamba sisi ni wepesi pia wa kusahau na kuunganisha matukio,kwani hata clouds radio kuna kipindi mwaka huu ilidaiwa watangazaji wamepigana studio(hapo ndo walitutambua watanzania maana tulisema tukamaliza maneno yote) lakini ikaja bainika baadae kwamba lile lilikua tangazo la kampeni fulani(wachache sana walioshituka kabla,ila wengi tulijua ni kweli wametwangana ndo tukaponda haswaa).
Wakati haujapita hata mwaka kijana amerudia kitu kile kile na kweli ametukamata,kwa hili nikaona niandike tuu huu Uzi ingawa utawachosha wengi.
Kwa kweli kuanzia leo mm najitoa ktk chama cha kukurupuka na shukrani zimuendee huyu kijana.
Nilikua mmoja wa mashabiki waliotaka kijana apigwe pale dodoma kwa kauli yake ya "dharau" juu ya legendary wa hip hop bongo HAYATI ALBERT MANGWEIR aka Ngwair.
Lakini naamini hata wakati ule pia nilikurupuka maana kwa hustle za HAYATI alizozifanya,jasho lake lilitakiwa lionekane hata sasa kwa familia yake...lakini mafisadi wachache ndio waliofaidika na jasho la hayati.
Kutokana na surprise hii ya huyu kijana nimejitoa rasmi timu kukurupuka.
NISAMEHENI KWA LI UZI REFU JAMANI.
NIMEWAWEKEA NA PICHA HIZI HAPA.
Asanteni.