Kwa hili la COVID-19 Hongereni Sana Manispaa ya Moshi

Kwa hili la COVID-19 Hongereni Sana Manispaa ya Moshi

Salam dm

Member
Joined
Apr 24, 2019
Posts
75
Reaction score
77
Ndugu zangu Watanzania tuko katika mapambano makali dhidi ya adui hatari aitwaye COVID-19

Kama tunavyoambiwa na wataalamu wa afya katika janga hili kuwa ni vyema kila akajikinga kwa kuchukua tahadhari zote muhimu.

Katika hili nawapongeza sana viongozi wa Manispaa ya Moshi kwa kuanza utaratibu wa kupiga dawa mabasi yote yanayoingia katika stendi ya mabasi ya Moshi. Uamuzi huu ni muhimu katika mapambano haya ambayo kimsingi lazima tushinde.

Tunapenda kuona hatua kama hiyo au zaidi ikichukuliwa pia na viongozi katika maeneo mengine.

Inshallah tutashinda vita hii.
 
Ni ujinga kama miujinga mingine.

Mkae mkitambua kuwa huu ugonjwa mpaka sasa hauna chanjo wala dawa wala kinga pia.

Sasa kupiga dawa ndani ya gari unategemea kuwa utakuwa unaua virusi vilivyo ndani ya gari au unataka kutuambia kuwa utakuwa utaua virusi vilivyo ndani ya miili ya watu?. Em amkeni Watanzania sio kila kitu tunapigia makofi tu.

Au wewe kwa akili yako iliyooza unategemea hapo anakengea nini?
 
Ni ujinga kama miujinga mingine.

Mkae mkitambua kuwa huu ugonjwa mpaka sasa hauna chanjo wala dawa wala kinga pia.

Sasa kupiga dawa ndani ya gari unategemea kuwa utakuwa unaua virusi vilivyo ndani ya gari au unataka kutuambia kuwa utakuwa utaua virusi vilivyo ndani ya miili ya watu?. Em amkeni watz sio kila kitu tunapigia makofi tu.

Au wewe kwa akili yako iliyooza unategemea hapo anakengea nini?
Atleast hata hawa wamejigusa kwa kupiga dawa kuliko bashite anayepiga siasa kwenye korona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom