somijo
Senior Member
- Apr 14, 2012
- 110
- 47
Siku zote dalili ya mvua ni mawingu, dalili hizi za kisiasa hapa nchini zinaonyesha vurugu, fujo, na utowevu wa aman katika siku za usoni. Tunajua CCM ndo wenye nchi kwa sasa, kwa maana mnashikilia dola mnatakiwa kujua kuwa Tanzania ya sasa si ya mwaka 1961, au 1977 au 1992 au 2005. Tanzania imebadilika jaman, CCM ongozeni kwa weledi wa wakati.
Kwa nini mnalazimisha vitu ambavyo watanzania hawataki!!!!!! Hiki kikombe cha fujo kikianza hakitachagua, huyu Ndughai au mwanaye, sijui huyu Mbowe au huyu ramadhani wa pale mwanakwerekwe, batamuzi wa ngara, au mwafilombe wa kajunjumele au huyu sijui huyu Hamy-D.
Sisi bado tunaihitaji aman ya nchi hii, hii tabia ya kutumia mabavu na kutumia vyombo vya dola kupitishwa matakwa yenu ya ubinafsi yenye mlengwa wa ufisadi kwenye katiba acheni. Hiyo katiba mnayolazimisha kuitengeneza haitokubalika na watanzania wengi na hebu fikirien mwisho wake utakuwa ni nini!
Kwa hili CCM mnaratibu kutowesha aman ya nchi; Hebu chonde chonde tumieni busara kwa hili.
""" Huo ni uono wangu wa mbali"""