instagramer
JF-Expert Member
- May 7, 2024
- 215
- 492
Ndugu wanaBodi...
Ni matumaini yangu mmemaliza salama majukumu yenu ya siku kwa uweza wa Mungu. Ila kwa wale wanaoingia nightshift basi ikawe Heri na watoke salama asubuhi.
Lengo la Uzi huu ni kuelezea changamoto niliyokumbana nayo Leo pale Kigamboni.
Nikiwa katika shughuli za Kila siku za kimaisha Kuna hii changamoto kubwa na inakera Sana ambayo nimekumbana nayo Leo.
Pale Kigamboni feri sehemu ya watu ku'scan N CARD Ili Milango ya kuingia jumba la kusubiria abiria ifunguke ni uozo mtupu, Tena uozo hasa. Leo jioni mida ya saa 12 kuelekea saa moja zile Mashine zote (upande wa Dar) zilifeli kufanya kazi. Na kusababisha foleni ya watu ambao kwa makadirio nadhani hata 500... Maana walifika mpaka mwanzo kabisa yanapokata tiketi magari au mbele kidogo. Hii ilikua kero kwa watu wengi na wengine kulalamika na kutaka kuvunja vile vigeti ili tupite (sababu wamekua wakifanya hivyo mara kadhaa zinapofeli) lakini kwa busara ya muhudumu mmoja aliamua kuachia mlango mmoja wazi watu wapite free..
Bashungwa, je katika hili huoni kwamba umefeli? Mmekosea njia Mbadala pale Mashine zinapofeli?
Ni mapato kiasi gani ambayo Serikali inapoteza pale mara kadhaa inapotokea kadhia hii?
Ulitembelea hapo siku chache zilizopita, hukuambiwa hili? Na kama uliambiwa ni hatua gani umechukua?
Ulipopiga mkwara kuhusu feni, dakika chache zikarekebishwa kwa kuwekwa mpya na kutoa za zamani. Lakini nikujuze, feni hizo hazitoshi hata robo. Zinahitajika feni nyingi Sana zifungwe mpaka katikati ya jumba na sio pembeni tu, wakati watu wengi wanasimama katikati.
Naomba kuwasilisha na naomba majibu!