Kwa hili la kubadili Cheti kuwa Stashahada kwa maslahi ya Kisiasa, Hapa Wizara ya Elimu imeboronga kabisa

Kwa hili la kubadili Cheti kuwa Stashahada kwa maslahi ya Kisiasa, Hapa Wizara ya Elimu imeboronga kabisa

Civilian Coin

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
2,305
Reaction score
4,380
WIZARA YA ELIMU IMEPWAYA KUFUTA MAFUNZO NGAZI YA CHETI NA KUIMARISHA DIPLOMA kwa MASLAHI YA KISIASA.

Ni Tanzania Pekee tu ndio isio jua umhimu wa NGAZI za Cheti na kukimbilia Diploma.

UMHIMU WA NGAZI YA CHETI.

Tulipofika elimu zote za NGAZI ya vyeti zitafutwa na kubaki na NGAZI ya Diploma. Hii Tanzania wanafikiri mkiwa na Diploma ndio mtaonekana Wasomi au mtaonekana mnatoa elimu Bora kumbe Bora elimu. NGAZI ya Cheti inatambulika Kimataifa na Nchi nyingine huwezi kupata diploma au degree bila kupitia NGAZI ya Cheti. Kwani NGAZI ya Cheti huwa wana soma vitu vingi. Mfano Mimi DON NALIMISON Leo nimekuwa Bora Kimataifa kwasababu kabla sijapata Digree mwaka 2012 nilipitia kwanza NGAZI ya Cheti Cha Uandishi wa habari mwaka 2003. Hivyo unapofuta NGAZI ya Cheti na kulazimisha Diploma maana yake ni kuwa umeshindwa kulipa Mishahara na hivyo huwezi kutoa nyongeza ya Mishahara Bali mmeona kufuta Cheti ili Walimu wapokee Mishahara ya Diploma Kama nyongeza ya kuhadaa kifikira.

KUFUTA CHETI NA KUHALALISHA DIPLOMA NI SAWA NA KUONGEZA MSHAHARA KIMYA KIMYA KWA KUWALIPA WALIMU MISHAHARA YA DIPLOMA.

Tuache kuhadaana, unyonge wa Walimu usiwe njia ya kuharibu Mfumo wetu wa elimu kwa kufuta elimu Mhimu ya Cheti kisa nyongeza ya kinyemela ya MSHAHARA wa diploma. Kinachofanywa na WIZARA ya elimu ni sawa na MTU ambaye hajaenda Shule kabisa. Nilitegemea Maprofesa wangeshirikishwa kwanza ili watoe dira ya elimu na sio hii ya kufuta Cheti kwa maslahi ya Kisiasa nasio kwa maslahi ya Taifa. Natutegemee kufuta Walimu wa Diploma sekondari na kubakiza Walimu wenye degree tu. Mahakama Kuna Mahakimu wa Cheti wengine diploma na wako vizuri hasa kuliko wenye degree. Lazima tutafakari kabla ya kutenda, Kama tumeshindwa KUONGEZA Mishahara Bora tuache Kama ilivyo kuliko kubadili Mfumo wa Kimataifa kwa maslahi ya Uchaguzi Mkuu wa 28 Oktoba 2020. Elimu ya Cheti ni ya Mhimu Sana, leo Serikali imeshindwa KUONGEZA Mishahara kwa miaka mitano iliyoisha, itawezaje kulipa ongezeko la Mishahara kwa kuwapandishia NGAZI ya Diploma. TAFAKARI MSITUHADAEEEEEEE.

Leo naomba niishie hapa:

DON NALIMISON
DON NALIMISON ADVISORY BOARD.
+255 682 94 29 01.
DAR ES SALAAM.
Screenshot_20201003-110402.png
 
Safi.....sindano imewaingia kwa hiyo hii inaanza lini?
 
Hii wizara sijui kwanini. Kuanzia mama Hadi maafisa elimu kata. Kama yule wa Mlele aliyemcharaza mwalimu fimbo zakutosha
 
Tulipofika elimu zote za NGAZI ya vyeti zitafutwa na kubaki na NGAZI ya Diploma. Hii Tanzania wanafikiri mkiwa na Diploma ndio mtaonekana Wasomi au mtaonekana mnatoa elimu Bora kumbe Bora elimu. NGAZI ya Cheti inatambulika Kimataifa na Nchi nyingine huwezi kupata diploma au degree bila kupitia NGAZI ya Cheti. Kwani NGAZI ya Cheti huwa wana soma vitu vingi. Mfano Mimi DON NALIMISON Leo nimekuwa Bora Kimataifa kwasababu kabla sijapata Digree mwaka 2012 nilipitia kwanza NGAZI ya Cheti Cha Uandishi wa habari mwaka 2003. Hivyo unapofuta NGAZI ya Cheti na kulazimisha Diploma maana yake ni kuwa umeshindwa kulipa Mishahara na hivyo huwezi kutoa nyongeza ya Mishahara Bali mmeona kufuta Cheti ili Walimu wapokee Mishahara ya Diploma Kama nyongeza ya kuhadaa kifikira.

Bora turudi huku maana kulitujenga vema kuliko wanakotupeleka sasa

IMG-20170901-WA0011.jpg
 
Back
Top Bottom