Kwa hili la Morrison, Simba mmewaumiza TFF makusudi

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Simba ni klabu kubwa na yenye heshima kubwa nchini na Afrika kwa ujumla, ni timu yenye historia iliyosheheni mambo mema katika nyanja ya burudani.

Lakini mbali ya ukubwa huo wa jina, bado Simba iko na itaendelea kufanya kazi chini ya Shirikisho la Soka nchini TFF kama mlezi na mwendeshaji wa shughuli zote za soka nchini.

Mgogoro kati ya mchezaji Morrison ulianza miezi kadhaa iliyopita na ulibaki Kama mgogoro binafsi unaozihusu Yanga na Morrison huku TFF akibaki mwamuzi asiye na upande. Ghafla Morrison akagoma kucheza Yanga akisema mkataba wake umeisha kwani ulikuwa wa miezi 6 pekee, lakini Yanga wakamshtaki Morrison TFF kupitia Kamati husika inayojihusisha na haki za wachezaji.

Yanga wakaambiwa wapeleke vielelezo vya mkataba wa miaka miwili (ambao ulishasajiliwa na TFF na CAF), na baada ya TFF kupokea nakala halisi (Original Copy) ya mkataba huo Wakamuita Morrison lakini akaukana.

Hivyo TFF wakalazimika kuhusisha vyombo vya uchunguzi wa kijinai (Polisi) ili isaidie kupata ukweli wa suala hili kama saini iliyoko kwenye mkataba ni ya Morrison kweli (genuine) au ni ya kughushi (forged).

Kabla majibu ya uchunguzi huo hayajatolewa hadharani na mamlaka mhusika (TFF), Jana likaibuka suala ambalo klabu yoyote makini isingeweza kulifanya. Akaonekana Morrison akisainishwa mkataba mpya na Klabu ya Simba, akavalia Uzi wa Simba na akaunti ya klabu ikaliweka tukio hilo kuonesha kuwa ni official event.

Hapa ndipo ninapolazimika kuwaambia Simba mmewaingiza TFF kwenye mtego ambao huenda ukawapa maumivu makali na wasieleweke kwa yeyote hata wakijitetea.

Nani ataamini TFF endapo watakuja na majibu kwamba mkataba ule ni feki kwa vile saini imeghushiwa iwapo tayari wapinzani wa mlalamikaji mnaonekana mnajua hukumu ya kesi kabla ya kusomwa rasmi? Watu wakisema (na wana haki ya kusema) kwamba TFF wamewapa kilichoko kwenye hukumu (wamevujisha) mtakataa? Kwa nini hata kama mlitaka kufanya, msingefanya jambo hili kimya kimya ili likija kinyume mnachana mkataba au likiwa upande wenu mnaibuka kwa shangwe?

Mmewezaje kufunga ndoa na mwanamke ambaye anadai talaka mahakamani na kesi inaendelea? Nani mwenye akili fupi kiasi hiki huko hadi anafyanya mambo ambayo yanatakiwa kufanywa na Lufinyo FC ya Madibila?
 
Umenikumbusha kuna shemeji yangu alishawahi kunihadithia alikua na mahusiano na Dada mmoja mara Dada akaanza vituko visingizo vingi jamaa akaona isiwe tabu akaamua kumkunjukia wakavunja mahusiano.Kikichotokea ndani ya wiki tatu yule bidada akaolewa.Jamaa akajua kumbe zote zile zilikua mbinu demu alikua kashaanzisha mahusiano mapya wakiwa pamoja.
All in all kuna funzo apa kwenye hili sakata.
 
Mfano mzuri sana, lakini Je, huyo muoaji alikuwa na akili sawa kuchumbia mke wa mtu?
 
Sidhani kama simba wamefanyi kijinga hivyo, wamefanya analysis na wanaujua ukweli. Simba na yanga ni watoto wa mjini wanajua mbichi na zilizoiva.
 
Sidhani kama simba wamefanyi kijinga hivyo, wafanya analysis na wanaujua ukweli. Simba ana yanga ni watoto wa mjini wanajua mbichi na zilizoiva.
Eti mtu wa JF alijue soka na vikolombwezo vyake vyote kuwazidi watu walioko pale Simba ahahaha itakuwa maajabu.

Tuwaache wajifurahishe na sie tuchangie as long as we know ni kupoteza muda tu
 
Kwa muktadha huu unataka kutuambia kwamba wakati Morrison akiwa Yanga alikuwa mchepuko wa Simba na kwamba ameolewa bila kuachika? Asante
 
Moderator huu uzi ushaandikwa sana humu kila mtu atafungua nyuzi za Morrison Bernard kama vile yupo yeye tu duniani? Tumechoka. Sisi yanga tutaumia yataisha ila tutalipiza tu.
Mtalipizaje?
Unaweza kuthibitisha huyo mchezaji ana mkataba na club ambayo huna hata kadi yake zaidi ya kupiga tu kelele?

Na kama itatokea alikuwa na mkataba na club unayoishabikia kuna conditions za mkataba ambazo zinasimamiwa na mashirikisho ya Soka zitaangaliwa.
Nikiandika kishabiki ilihali mimi ni mwanachama wa Mnyama ni kwamba haya ni malipo ya Kessy na Mbuyu Twite.
 
Utopolo mnahangaika na morison ambae hawataki ajabu sana, nyie ni tasisi sajili ata mess au mbape aje Yanga.

Tulieni tukawatafutie nafasi ya viti maalum mwakani na nyie mshiriki club bingwa, maana mnaweza kaa miaka 10 bila kushiriki
 
Sidhani kama simba wamefanyi kijinga hivyo, wamefanya analysis na wanaujua ukweli. Simba na yanga ni watoto wa mjini wanajua mbichi na zilizoiva.
kiufupi soka la Tanzania ni la kipumbavu
 
Ata kama mchezaji hakua amelipwa chochote na Yanga uo mkataba alio saini bado haujavunjika kwakua mkataba ni nyaraka ya kisheria,kwakua shauri Lao liikua lipo Tff. Yaani kama ni ndoa ata kama mwanamke alikua amekwenda kushtaki kunyanyaswa na mumewe kwakutopewa fedha ya matunzo na wasuluhishi (Tff) hawajalipatia ufumbuzi, Chaku shangaza mwenyemke (yanga) alisha toa malalamiko Tff kama angalizo mkewe (Morrison) Kuna jirani anamfukuzia. Kabla usuluhishi hajapatikana jirani anatangaza kashafunganae ndoa kwakua mwenyemke alikua hatimizi mahitaji yake.
Mkiambiwa mbumbumbu fc un educated mnabisha. Mwachieni Manara akafundishe Madrassa aya mambo ya mpira hayaitaji mikurupuko.
Kama Tff watashindwa kuishusha Simba daraja nitashangaa sana kwakua nijambo ambalo lilisha pelekwa na yanga kama lalamiko kua simba inamrubuni Morrison tena kwa barua rasmi ya malalamiko, Bila woga Uongozi wa Simba umemtangaza Morrison ka imemsajili kwenye Official page ya club sasa ata ilo Tff itahitaji uchunguzi? Jumatatu tunatarajia kilakitu kitamalizwa kabisa kwakua ushahidi umeshakamilika.
 
Tff ndio wababaishaji wewe kujua kuwa sahihi hii ni ya kufoji ndio muda wote huo? Zipo case nyingi nyingi kama chuji hadi leo suala lake kama hili halijapatiwa majibu!! Kuhusu kujua hukumu, kwani hizo kamati za tff zinaundwa na kina nani?, wao simba je kama wamejilipua tu kuwa sisi tumemuamini morison kuwa amesema hana mkataba, yupo free hayo mengine hayatuhusu, kama tumeingia choo cha kike basi tutawajibika kwa hilo!! Hapo unasemaje. Ila kwa kinachoendelea viongozi wa yanga wanajua picha yote, hivyo ni kuwaadaa tu mashabiki wao!! Na tff hata kama akija na hukumu ya kumpa ushindi morison hakuna shida kwani, kesi si ni ushahidi?
 
Kwa taarifa tu ni kuwa Simba wamesha ziondoa zile picha kwenye page yao, tangu usiku kwenye Instagram.

Ila watu wamewastukia na wana zirudisha kwenye individual page ili ushahidi uendelee kuwepo na mchezo wote wameucheza kina Hanspope na Magori
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…