Kwa hili la urudishaji wa mikopo naona halijakaa sawa!

Kwa hili la urudishaji wa mikopo naona halijakaa sawa!

Ubumuntu

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
14,345
Reaction score
10,885
Salaam wanaJF!

Kwa wale waliosoma vyuo vikuu hapa Tanzania haswa wakati utaratibu wa mikopo kupitia bodi ya mikopo, wataelewa hili jambo. Wakati wa kuingia mkataba na bodi, mkataba ulisema kwamba utaratibu wa kurudisha mkopo utachukua kipindi cha miaka 10 tangu uanzwe kukatwa. Sasa leo katika taarifa ya habari ya TBC1 nimemsikia waziri wa elimu akisema bodi imebadilisha utaratibu (ingawa taarifa yenyewe ilikua fupi na isiyo na mwanzo na mwisho) kwamba bodi sasa itakua ikikata asilimia 8 ya mshahara wa mdeni!

Sasa nimejiuliza, hivi bodi imetumia utaratibu upi wa kisheria kubadilisha utaratibu bila kumhusisha mteja? (alieingia nae mkataba wa kupata mkopo)

Wanasheria mnaweza kunisaidia katika hili tafadhali.

Asante.
 
Hvi kumbe huwa zinalipwa kweli?

Zinalipwa kweli mkuu..mimi nakatwa kila mwisho wa mwezi Tsh. 50,300! Kwenye mkataba waliniambia ninapaswa kuwalipa kwa miaka 10 lakini nashangaa sasa wanakuja na kusema ninapaswa kuwalipa kwa kipindi cha miezi 65! Mbona hawajazingatia mkataba?

Ndio maana naomba msaada wa wanasheria!
 
Nafikiri ingebidi yawe makubaliano. Ila kama unajiweza kalipe tu deni lote watoto wasome.
 
Back
Top Bottom