Kwa hili la VAT, Mkurugenzi mkuu wa NHC - Bwana Mchechu umechemka

Kwa hili la VAT, Mkurugenzi mkuu wa NHC - Bwana Mchechu umechemka

Congo

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2008
Posts
2,081
Reaction score
2,325
Jana wakati naangalia vyomba vya habari ulinukuliwa ukisema kuwa wanunuzi wa nyumba mnazojenga waondolewe kodi ya VAT wakati wa ununuzi wa nyumba hizo hasa wale wanaonunua za bei chini ya shilingi milioni mia moja. (milioni mia moja!!!!!!!!!!!!!!!!!!). Kwa hili ninasema umechemka. Nina sababu kadhaa za kuamini hivyo. Kama mtu anaweza kudiriki kupata milioni mia au pungufu kidogo huyo sio mlalahoi. Ni mtu mwenye kipato kikubwa ambaye anastahili kabisa kulipa kodi ili serikali iboroeshe miundombinu ya nchi. Kuna watu wanadunduliza kidogo kidogo, wananunua mfuko mmoja wa saruji, bati mojamoja mpaka wanafikia kujenga kibanda ambacho tathmini yake haifiki hata milioni kumi. Watu hao wanakuwa wamelipia VAT kwa kila kifaa cha ujenzi wanachonunua. Je, utawasaidiaje na wao wasilipe kodi ya VAT kwa vifaa wanavonunua? Mjenzi mkubwa wa nyumba nchi hii sio NHC ni wananchi wenyewe. Wananchi wamekuwa wakilipa VAT kupitia ununuzi wa vifaa vya ujenzi. Hawa wanaonunua nyumba hizi hawanunui vifaa vyoyote vya ujenzi, wewe unataka wasamehewe kodi. Lo!!!!!
Ulizingumzia kwamba watakaokopa benki watakopa pamoja na mkopo wa kulipia kodi ya VAT. Wewe ulikuwa Mkurugenzi wa benki, Je, ulipokuwa unaletewa mchanganuo wa kuomba ununuzi wa vitu ambavyo vinalipiwa VAT ulikuwa unakataa kutoa mkopo unaolipia VAT? Ninajua kuwa wanaokuja kukopa banki kwa haraka (mkopo wa mwezi mmoja) huwa mara nyingi wanakopa ili kulipia kodo mbalimbali ili kukomboa bidaa zao kutoka kwenye mikono ya watoza kodi. Je, ulikuwa unawanyima hao mikopo? Umeanza lini kuwa mwanasiasa?
Bidhaa nyingi tena muhimu tu zinatozwa kodi ya VAT. Mchele, ngano, nguo za mitumba za walalahoi wasioweza kununua nyumba unazojenga na kadhalika. Bidhaa hizi ni muhimu kama nyumba unazojengea wenye kipato kikubwa maana hakuna mtu yeyote mwenye kipato kidogo atakayekuja kununua nyumba unzojenga. Heri NSSF, wao kidogo wanjengea wanachama wao kwa bei nafuu.
Nimepanga ofisi kwenye nyumba yako. Ni maumivu matupu.
Kwa heri kwa leo.
 
Congo,

Mchechu yuko sahihi. Serikali ina wajibu wa kuwawezesha wananchi wake kupata sehemu za kuishi. Vifaa vyote vinavyotumika kujenga nyumba vimellipiwa kodi. Kwahiyo iwapo serikali itaondoa kodi kwa wanunua nyumba haitapata hasara yoyote.
 
Back
Top Bottom