Kwa hili la vigezo vya wachezaji wa kigeni, kamati ya utendaji-TFF inastahili pongezi

Kwa hili la vigezo vya wachezaji wa kigeni, kamati ya utendaji-TFF inastahili pongezi

Yethero Mgale

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Posts
525
Reaction score
228
Katika kikao cha kamati ya utendaji ya TFF kilichofanyika hii leo Zanzibar, pamoja na maamuzi mengine, kamati hiyo imeweka vigezo kwa wachezaji saba(7) wa kigeni wanaopaswa kusajiliwa na klabu za ligi kuu ya Tanzania, vigezo hivyo ni:
1. Lazima mchezaji huyo awe anacheza timu ya Taifa ya nchi hiyo (senior team au U17 au U23)
2. Awe anacheza klabu ya ligi kuu anakotokea.
My take: hili litasaidia kukomesha usajili wa wachezaji wanaokuja kujifunzia soka kwenye hivyo vilabu
 
Safi sana, waleteni wenye kucheza mpira sio wanaokuja kujifunza mpira
 
vigezo viko poa sn, ila hili la kusema wakigeni ruksa kufikia 7 sijaliafiki hata kidogo!
Kwa afya ya timu yetu ya taifa, hapa tutaloose kwa asilimia kubwa maana vilabu vikubwa simba, yanga na azam ndio wanatoa wachezaji wengi wa Taifa Starz na ndio timu mbili kati yao wachezaji wao wanapata exposures za kushiriki internationl clubs leagues. Pia hizi timu ndio zinaongoza kwa kusajili mapro hivyo hali hii itachangia kuidumaza timu yetu ya taifa!!

TFF ilitakiwa iidhinishe wachezaji mapro wasiozidi 3-4 tu!
 
Back
Top Bottom