Kwa hili la vita dhidi ya ukabila, jameni tuwaige Watanzania

Kwa jinsi watanzania karibu wote humu JF wanavyopinga hoja yako, ni dalili tosha kwamba yale yote niliyokueleza kuhusu ukabila Tanzania na jinsi Nyerere alivyoufutilia mbali ni sahihi, sasa kwa kukusaidia zaidi, ukitaka kuifahamu Tanzania vizuri sana, jaribu kujiuliza maswali yafuatayo
1)Tanzania, kama zilivyo nchi zengine zote za ukanda huu, ukabila ulikuwepo hata kabla ya kuja kw wakoloni, je nani aliwaunganisha watanzania na kumaliza ukabila?, waarabu, mjerumani, waingereza, Nyerere, au wananchi wenyewe tu walijikuta wanakuwa kitu kimoja automatically?
2)Kiswahili kilizaliwa katika pwani ya Afrika mashariki, je ilikuwaje kiswahili kienee na kupenya kwa kasi huku Tanzania lakini kisiweze kupenya huko Kenya, ni nani hasa aliyekieneza Tanzania na asifanye hivyo huko Kenya, au Mungu anaipendelea zaidi Tanzania kuliko Kenya kwa kueneza kiswahili Tanzania ambayo ilikuwa ni silaha muhimu kufuta ukabila?
3)Kama hoja yako ya kwamba mkoloni hasa wa uingereza hakuona umuhimu wa kutugawa, lakini kumbuka alitukuta tumeshagawanyika kutokea enzi za mababu zetu, je nani alituunganisha kama muingereza hakuona umuhimu wa kutugawa zaidi?
4)Kwanini Rwanda na Burundi ambao pia waliwekwa chini ya uangalizi wa Belgium, ambaye hakuona sababu ya kuwagawa kama Tanzania, kwanini wanaendelea na ukabila wao uleule wa kabla ya kuja kwa wakoloni?
 
Leo nimepata muda na kuisoma kwa undani hii habari, kwanza nianze kwa kusema kwamba, MK254 wewe ninahisi unao uwezo mkubwa wa kuweza kusoma habari na ukaichakata na kujua huyo muhandisi ni mtu wa aina gani, sitegemei habari kama hii unaweza kuitumia kama habari rejea kwako ili kuipa nguvu hoja yako, you are much better than this guy.

Inaonekana huyu jamaa huko Europe alikoishi wazungu walimnyanyasa sana kiasi cha kujenga chuki iliyopitiliza kwa wazungu, pia amekuwa ni mtu mwenye kutoa lawama hovyo siziso na references zozote zile zaidi ya kusema mambo aliyoyasikia tu, hayo yote ya kwamba Afrika ndiyo watu wa mwanzo duniani kuwa na vyuo vikuu, kufanya operesheni ya uzazi, kutengeneza mashua, kuanza kuhesabu, ni maneno tu aliyoambiwa na watu hana ushahidi wowote ule, nimeshangazwa sana na wewe kutumia habari hii kama reference yako, unajidhalilsha sana, labda nizungumzie kuhusu hili la kwamba watanganyika walifuta ukabila na Kiswahili kilienezwa na train enzi za mjerumani,
1)Kenya ndiyo iliyoanza kujenga reli toka Mombasa kuelekea Nairobi hadi Uganda, kwanini Kiswahili kisienee Kenya hadi Uganda kama train ndiyo iliyokuwa sababu ya kueneza kiswahili?
3)Kwanini mjerumani awaunganishe watanzania pekee lakini ashindwe kuwaunganisha Rwanda na Burundi kwa kuwa wote walikuwa chini ya koloni la mjerumani ikijulikana kama The Germany east africa?

Ninarudia kusema, I hope you are better tha this man, don't downgrade your self please
 
Kwani wewe ni wa kabila gani? Tunamjua kama mtanzania tu. Kwani tunatambika. 35% ya watu wa TANZANIA tumeona makabila tofauti. Na karibu makabila yatapoteza lugha zao. Watoto awajui tena lugha zao
 
Umeeleweka ila nina wasiwasi sana maana lugha yako kiswahili chako na uandishi wako hauoneshi hata chembe ya ukenya inaonesha ww kijana wa mjini tu hapa Tz.
 
Kenya hamna ukabila, shida ni ukikuyu na ukale vidi ya Wakenya
 

tupe taarifa ya utafiti wako ambayo inaonesha waTanzania hawapendi kusoma.
 
Vita dhidi ya ukabila vianze kwetu sisi huku mashinani, nina uhakika viongozi wataishia kutuunga mikono, lakini kama tukiishi kuwasubiri hao waje na sera zozote, watakua wanatutumia kama mtaji.
Suluhisho ni kutengeneza sheria kali za kuzuia ukabila na vitendo vyake kama alivyofanya kagame
 
sipati picha mngekua tribes nyingi kama sisi........nadhani kenya pangekua moja yamaeneo yetu yakuchungia mifugo tu........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…