Kwa hili, Messi na Mashabiki wako mnatudanganya sana

Wewe unavuta bhangi? Mimi ni liverpool fan lakini shughuli ya messi naifahamu pia ukizungumzia hivyo tutajie mchezaji mmoja tu ambae yeye kila mechi alikuwa anafunga
Ya nini mchezaji kufunga kila mechi. Kucheza na La masia wenzio kwa zaidi ya nusu ya umri wako wa kisoka na walio wahi kuwa bora kabisa duniani eneo la kati ni advantage kubwa. Mchezaji mvivu uwanjani kama Messi, ametembelea uwezo wa timu kwa muda mrefu. Fuatilia hizo takwimu za kombe la dunia lililopita kujua anauwezo(coverage) gani uwanjani bila walishi wake. Kipa Lloris alimzidi distance covered kwa mechi moja.

Sasa akiangali umri na wale wa kumng'arisha hamna, anaongea kuliko muimba taarabu bongo.
 
Nishskusoma sasa kumbe wewe ni mnazi wa CR7 maana mapungufu ya CR7 unaibebesha timu nzima ila mapungufu ya messi unamwachia messi mwenyewe, mimi nataka unitajie vitu viwili tu? G.O.A.T wako ni nani na ni ipi club kubwa haijaonja joto la messi
 
Kwa taarifa yako hiyo barca ya kuanzia 2010 hadi sasa inamuhitaji messi kuliko messi anavyoihitaji barca
 
Kwamba Messi ni mzigo? Huu uzi mzima umeuleta kumjadili mtu wa miaka 33? Haya hebu lete uchambuzi wako juu ya magoli 90 aliyofunga ule msimu.
Maradona kafunga magoli 100 Tu huko Napoli..
Messi anafunga magoli 700 unaleta story za maradona?

Enzi za maradona hata kupaki basi ilikuwepo?
 
Kwa taarifa yako hiyo barca ya kuanzia 2010 hadi sasa inamuhitaji messi kuliko messi anavyoihitaji barca
Eti eeeh? Messi ni bora kuliko the rest of the team sio? Kweli lakini
 
Nishskusoma sasa kumbe wewe ni mnazi wa CR7 maana mapungufu ya CR7 unaibebesha timu nzima ila mapungufu ya messi unamwachia messi mwenyewe, mimi nataka unitajie vitu viwili tu? G.O.A.T wako ni nani na ni ipi club kubwa haijaonja joto la messi
Mbona nimekubali kuwa hata ronaldo pia ana hali mbaya mkuu mbona unajaribu kuleta uteam kwenye huu uzi. Unanijengea mazingira ya mimi kuonekana team ronaldo mkuu
 
spot on mkuu, niliwahi kuleta stats nyingi humu kuanzia fainali za copa america, world cup, hatua za champions league etc, jamaa yupo vizuri sana kuzifunga timu ndogo na huwa anapotea sana kwenye big stage, tafuta statistic za magoli yako uefa makundi, round ya pili, robo, nusu na fainali utaona anavyopotea jinsi unavyokwenda juu, anawaonea tu Man u na Arsenal basi.
 
Wewe jamaa ni hatari. kiukweli unafuatilia mambo.
 
umetusaidia kumjibu huyuu muanzisha mada
 
Mkuu umeongea mkuu inabidi niitafute hiyo thread mkuu
 
Ambae hapotei ni nani?
 
Nitajie club kubwa duniani ambayo unadhani messi hajaifunga


Kwa upande wa vilabu Madrid ndio club iliyochukua UCL mara nyingi ila rekoci zinaonyesha messi alishawapiga hatrick zaidi ya moja. Kwa level za nchi brazil ndio taifa lililochukua combe la dunia mara nyingi lakini Messi ashaifunga brazili hatric. Messi ndie mchezaji aliyevifunga vilabu vya EPL magoli mengi zaidi UCL. Akija mtu akasema anafunga viloabu vidogo inabidi kwanza atutajie mchezaji mwenye magoli mengi dhidi ya vilabu vya EPL UEFA au atuambie kua vilabu vya EPL ni vidogo ndio maana ameongoza kwa kuvifunga, au atuambie Madrid na brazil alizofunga hatrik kama na zenyewe ni ndogo.
 
Messi amewahi kuwafunga Brazil when it Matter? swali lipo hapo, mechi za kirafiki hata 100 ukifunga inasaidia nini? unajua fainali ngapi za Huko kwao copa America ameflop?

na hata hivyo vilabu vya uingereza mechi pekee ambayo nakubali amefanya makubwa ni fainali na Man utd, akikutana na vilabu vya uingereza hatua ngumu kama robo na nusu pia ana struggle, tumeona na liverpool, chelsea mara 7 mfululizo, man United nusu etc. nenda kwa bayern, juve, atletico (uefa) etc. mfano hao Atletico wakicheza La liga Messi unamuona ila wakikutana mechi YEnye pressure kama Uefa Barca wanaanga mashindano, hapo ndio unaona tofauti ya ma legendary wa zamani na wachezaji wetu hawa wa sasa.
 
Mkuu hattrick nayoijua mm ni moja tu tena ni friendly match(4-3) sasa sijui unasemea ipi labda unikumbushe.

Af pia sawa messi anafunga ndio lakini hafungi mechi zenye impact.

Mechi kubwa za muhimu chukua mfano hata hizi knock out stage tu za uefa. Kama ni hivyo anafunga ndio usingekuwa mwaka wa 5 huu bila UEFA.

Cha kushangaza ni kwamba messi anamagoli mengi kwenye group stage halafu knock out ni madudu tu. Hii tafsir yake ni kwamba messi ni bora akikutana na weak teams na sio big teams na kwenye mashindano makubwa

messi kufunga team kubwa we mwenyewe unajua kama ni hivo basi tungeona ni kawaida messi kuchukua uefa, kuzifunga team za england haishtui team zenyew si hizi arsenal na man u
 

Nitajie mchezaji mwenye magoli mengi dhidi ya vilabu vya EPL anaemzidi.
 
Nitajie mchezaji mwenye magoli mengi dhidi ya vilabu vya EPL anaemzidi.
Alan Shearer? Ana magoli zaidi ya 200?

Na hili sio dhumuni la mtoa mada, hapa anazungumzia Messi anafunga mechi rahisi, mechi ngumu Hafungi, kumfunga Arsenal round ya pili ni tofauti na kumfunga liverpool nusu.
 
hahahahaha ukumbuke
2009 Barcelona vs United Man
Messi akatia kamba fainali hiyoo
2012 Barcelona vs Man United
Messi katia kamba fainali hiyooo
kawafunga Arsenal, Liverpool, Madrid, Munich, kwenye hatua za robo mpaka nusu fainal
kiufupi Messi ni miongoni mwa mafundi wa kandanda kuwahi kuwaona duniani
 
Acheni longolongo tumewaambia tutajie timu kubwa ambayo haijafungwa na messi lakini hamtaji mnabaki kuzunguka tu, nikwambie nusu fainali iliyopita messi katupiga liver goli mbili au nusu fainali ni group stage?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…