Kwa hili, Mungu azidi mkumbariki William Ruto

Kwa hili, Mungu azidi mkumbariki William Ruto

The Genius

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
822
Reaction score
2,095
Huyu mtoto anaitwa Cherono William Samoei Ruto. Alizaliwa huko Machakos lakini akatupwa akiwa na siku moja tu. Haijulikani sababu ya kutupwa, huenda ni ugumu wa maisha kwa wazazi. Alipotupwa alifunikwa na udongo lakini sehemu ya kichwa ilibaki wazi.

Mfugaji mmoja alipita na mifugo yake na kumuona mtoto amefunikwa na udongo analia. Akaita wananchi wenzie wakamnyanyua na kukuta ameanza kuliwa na funza kutokana na kutupwa eneo lenye uchafu.

Wakambeba na kumpeleka kituo cha kulelea yatima cha Madre Ippolata Children's Home kinachomilikiwa na masister wa shirika la moyo mtakatifu wa bikira Maria wa Kanisa takatifu Katoliki la mitume.

Masister wa Madre Ippolata wakampokea na kumpatia matibabu kisha kumlea katika kituo hicho pamoja na watoto wenzie. Wakampa jina Nadia wakimaanisha Tumaini (Hope).

Mwaka 2015 Rais mteule wa Kenya (wakati huo akiwa Naibu Rais), Willium Ruto alitembelea kituo hicho akapewa simulizi ya mtoto huyo. Ikamgusa sana. Akaomba kumuasili (adopt) na kuruhusiwa. Akafuata taratibu za kisheria za kuasili mtoto na alipokamilisha akamchukua na kuishi nae. Akampa jina Cherono ambalo ni jina la mama yake mzazi.

Ruto amemuweka Cherono katika orodha ya watoto wake, na hivyo kufanya idadi ya wanae kuwa 7 baada ya wengine 6 aliozaa na mkewe Rachel.

Akizungumza sababu za kumuasili alisema "Habari ya mtoto aliyetupwa na kufukiwa sehemu ya mwili wake, akiwa kichanga wa siku moja ilinigusa sana. Sikujua kwanini malaika huyo asiye na hatia alifanyiwa ukatili mkubwa kama huo. Hivyo niliamua kumuasili na kumpa jina la mama yangu, Cherono, na kumfanya sehemu ya familia yangu. Kila napomuona ni kama nimemuona mama yangu"

Kwa sasa Cherono ni mtoto wa Rais. Atapata haki, hadhi, heshima na stahiki zote zinazompasa mtoto wa Rais. Yamkini wazazi wake wanatamani kumwambia sisi ndio tulikuzaa tukakutupa, lakini hawawezi kufanya hivyo maana watatiwa hatiani kwa jinai.

Hivi ndivyo Mungu awezavyo kubadilisha maisha yetu kwa njia tusizotarajia. Biblia inasema yeye humwinua mnyonge kutoka mavumbini, humpandisha maskini kutoka jalalani na kumketisha pamoja na wakuu (Zaburi 113: 7-8). Na hakika maandiko hayo yamejidhihirisha kupitia Cherono. Utukufu kwa Mungu.!

Malisa GJ
FB_IMG_1660711129127.jpg
 
Heko sana kwa mke wa Mheshimiwa huyo.

Heko sana Rais, pengine hicho kitendo cha kumchukua huyo mtoto ndicho kimekuinua kufikia hapo.

Huku kwetu wajifunze, siyo kuwapelekea pipi na biskut tu, wachukueni wengine mkae nao.
 
Back
Top Bottom