Ni kuhusu swala la Polisi wetu kukamata watu kihuni. Mara nyingi tume shuhudia Polisi wakikamata watu kihuni, hapa sizumgumzii mambo ya utekaji nyala, isipokuwa ule ukamataji wa kawaida labda mtu anahisiwa kuwa mwizi na makosa mengine. Polisi wa nakuja na gari lina namba ya nchi za nje hasa South Africa na Singapore. Polisi wamevaa Jeans wana rasta na mizula kichwani, serikali ya Mtaa haina habari wala mjumbe wa nyumba kumi hana habari. Sasa imetosha serikali iseme hadharani kuwa ni marufuku Polisi kwenda kwa mtu iwe usiku au mchana kumueka chini ya ulinzi na kuondoa naye bila kuwepo uongozi wa serikali ya Mtaa au kitongoji na mjumbe wa nyumba kumi. Na pawepo kitabu/Register ambapo kiongozi wa operation hiyo ataandika jina jake kamili na cheo chake, sababu za kutaka kutaka kuondoa na mtuhumiwa na anapelekwa kituo gani. Na lazima wawe na vitambulisho halali vya kazi na ikiwezekana vya NIDA kwani vya kazi anaweza kughushi. Mbowe umesema Ukweli kuwa tunashikwa ' Kihuni na Kiboya'. Itoshe kusema Watanzania tupaze sauti imetosha.