Kwa hili nimekukubali

peter tumaini

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
573
Reaction score
94
Habari wanabodi,

Jana Jumapili nilipokuwa nafuatilia taarifa ya habari ya ITV,nilifarijika kwa Mmiliki wa Makampuni ya IPP kutamka kuwa atayaorodhesha makampuni 2 pale DSE kwa hiyo watanzania wanunue share na kupata umiliki,hii kiuchumi iko njema na inaimarisha soko la mitaji na ndo chanzo kizuri cha kokomaza uchumi wa ndani iwapo wajasiliamali waliopiga hatua watajitokeza na kuorodhesha makampuni yao katika soko la hisa ili tukuze sector.

Na pia aliwaahidi wafanyakazi watapewa fursa ya kununua hisa kwa utaratibu maalum na akapandisha mshahara na kima cha chini kitakuwa tshs.450,000/ kwa wafanyakazi wa IPP.Hii inaboresha kipato kwa watanzania na kuongeza Purchasing power.

Kwa hili Reg Nimekukubali umetoa special economic stimuli.

Nawasilisha.
 
Tusubiri, tuone hali ya soko na mwenendo wa bei ya hisa. Si unakumbuka ile NIKOL ya Felix Mosha na wenzie.... Big up Mengi, IPP itakuwa mikononi mwetu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…