Ukijenga nyumba na kukaa hapo kwa muda mrefu, kisha baada ya miaka barabara ikachongwa na kupitia karibu sana nyumba hiyo kiasi cha kuacha hatua chache. Hapa sheria inasemaje kama nyumba hii sasa haipaswi kuwa hapo kulingana na nafasi kati ya barabara na nyumba? Na hatua gani ninapaswa kuchukua? Wanasheria mtusaidie. Steve.
Si kosa barabara kupita karibu na nyumba, ila ni kosa kujenga ndani ya hifadhi ya barabara. Kumbuka kuna aina mbali mbali za barabara na kila moja ina vipimo vyake vya umbali kutoka makazi ya watu, kuna barabara za mtaa mpaka high way.
Kama nyumba ilikuwa kwenye eneo lililotengwa kwa ajili ya barabara, then options zako zitakuwa very limited. Kama lilikuwa sio eneo la barabara, then unatakiwa ulipwe fidia.