Wa Mjengoni
JF-Expert Member
- May 4, 2010
- 480
- 128
Mara tu bada ya kupata ushindi wa kishindo kwenye kinyanganyiro cha kihistoria cha Uenyekiti wa BMK, Mh. Mzee Sitta akitoa hotuba ya shukrani alisema atawashughulikia wanaopinga Muungano. Leo gazeti moja limemripoti Mh. Mchungaji Mtikila akijibu mapigo kuwa Sitta asithubutu kuzuia hoja zake la sivyo ataangukiwa na "hiroshima".
My take hapa ni kwamba je ilikuwa ni busara kwa Mh. Sitta kutangaza waziwazi atawashughulikia watu wa aina hii? Kulikuwa na haraka gani kungoja akiwa kitini na kuwashughulikia kama anavyosema?
Kwa kidemokrasia ya mawazo huru ninavyoelewa mimi hao wapinga muungano, wa serikali 1, wa2 na wa3 wote ni watu wake wamo humo Bungeni yeye akiwa Mwenyekiti, sasa kulikuwa na haja gani ya kujipambanua waziwazi hawa wa muungano atawashughulikia!
Namwombea Mungu Mzee Sitta ajazwe hekima, tusianze vibaya.