Kwa hili suala la Abdala Shaibu (Ninja) linanifanya niamini kuwa Yanga sc Kuna viongozi wazembe na wanye dharau

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
BEKI wa Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja' ameweka wazi sababu iliyomfanya akae jukwaani miezi sita baada ya kutoka Dodoma Jiji kwa mkopo ni kuchelewa kwa barua yake ya uhamisho.

"Taratibu zangu za uhamisho kurejea Yanga hazikukamilika, hivyo ingekuwa ngumu kuanza kucheza," alisema Ninja ambaye hajaonekana kwenye mechi yoyote ya Yang a inayokabidhiwa ubingwa kesho Ijumaa, Jijini Mbeya dhidi ya Prisons.

Meneja wa Yanga, Walter Harrison alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya Ninja ingawa hakufafanua kiundani; "Kulikuwepo na changamoto hiyo."

Source Mwanasport.

My take: huu ni uzembe wa hali ya juu mchezaji kuwekwa nje miezi sita (6) Na hii inadhihirisha wazi Yanga Kuna viongozi wenye Dharau laiti Kama Feisal salumu angeamua kufunguka tungekimbiana.

Viongozi wa Yanga sc mnapaswa kubadilika na ndiyo maana mchezaji Kama Morrison anawechezea sana na hamumfanyi chochote maana akili zenu alishazisoma.


 
Inaonekana kuna viongozi pale Yanga wanamkubali sana huyu mchezaji. Au ndiyo yale mambo ya 10%!!

Maana hata ufanisi tu uwanjani wa huyu mchezaji kwa timu kama Yanga, sijawahi kuuona. Akicheza pale nyuma, muda wowote anasababidha penati, kutokana na matumizi yake makubwa ya nguvu kuliko akili!

Kwa nini wasimalizane naye, ili akatafute changamoto mpya mahali pengine? Uwezo wake hauna kabisa tofauti na ule wa Abdulaziz Makame "Buyi". Ni average players.
 
Km anahitaj kuchangiwa pesa ili aende cas asiwe na presha sisi tupo paleee tunasubir namb
 
Kweli kabisa mkuu kuliko kuanza kumbabaisha ni uonevu tu.
 
Km anahitaj kuchangiwa pesa ili aende cas asiwe na presha sisi tupo paleee tunasubir namb
Yeye hajaomba pesa Ila kweli kukaa nje bila kucheza hata mechi moja NI kuua kipaji kwa makusudi kwa kweli
 
Upo sahihi na vile vile yanga ina wachezaji 28 badala ya 30 ukichanganya na huyu , doumbia na bigirimana kuna gap ya wachezaji 5 muhimu ambao Kama yanga angesajili vifaa vya maana angechukua Hata CL au kufika final .
 
Hakuonekana kuwa mhimu, kikubwa ashukuru analipwa mshahara wake na maisha yanaendelea....
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sasa si angerudi huko Dodoma jiji kucheza ball, km uhamisho hauku kamilika, woiiiiiii
Angerudije kucheza Dodoma jiji wakati muda wa mkataba wa mkopo ulishaisha.
 
Nadhani ni kwa sababu wanaona hana umuhimu,kwa sababu wapo kina bacca na beka,wangeumia hao wangejua hawajui..DHARAU SANA HAO WATU .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…