Kuhusu wasanii kunyonywa, hasa na hawa clouds.....naungana nanyi kabisa kwenye hili.
Nani asiyekumbuka jinsi wasanii walivyokuwa na maisha mazuri kabla ya ujio wa clouds wanyonyaji. Enzi za redio adilifu RTD. Wasanii kama marehemu Marijani, Mbaraka, Balisidya, Niko zengekala na wengine waliona matunda ya kazi zao. Vipi kama clouds wangekuwepo enzi zile. Pia tukumbuke ujio wa REDIO MOKO chini ya watangazaji mahiri Mzee Chaz, Nyaisanga na wengine, jinsi walivyoibuka wasanii kama Muumini(kocha wa dunia), Banza (mwalimu wa walimu), Mhina Panduka(Toto Tundu), Omary mkali, Misambano, Sonyo na wengineo, jinsi walivyofaidi manufaa ya kazi zao kwa kuwa tu haya majamaa ya clouds hayakuwepo. Juzi nimesikia eti Diamond ana bilioni moja tu kwenye akaunti. Wizi mtupu.....Diamond ni wa kuwa na hela chache hivyo kweli...Na ukiona hivyo ujue clouds wamepiga bilioni moja kutoka kwake. Tuungane tuitokomeze clouds tuone matunda ya muziki wetu. Turudi enzi za RTD, Redio moko n.k. Mtafaidi kama walivyofaidi kina Bichuka, Dede, Ngurumo, Zahiri Zoro,Bakule, Ndada na wengine.........Eti Diamond ana bilioni moja...Tuing'oe clouds muone akaunti za kina mzee Makasy, Tongolanga,Chimbende ....zitakavyosoma.
KUJIUNGA NA HARAKATI HIZI WASILIANA NA MH MISTA MBILI.