Kwa hili wasanii wa bongo mtakuwa omba omba mpaka mtakapoingia kaburini

Joined
May 28, 2013
Posts
91
Reaction score
17
Wasanii wa Tanzania hususa hawa wa bongo fleva mmekosa hata kuanzisha mfuko wenu wa kusaidia mpaka mnafikia hatua ya kuomba rambi rambi kwenye media si vibaya kufanya hivyo inabidi mjifunze sasa MUANZISHE HATA CHAMA CHENU..
 
Ushauri mzuri lakini sidhani kama utafuatwa. Wamekalia bifu tuu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Clouds ndo wanajua na exploitation policy yao
 
ni ushauri mzuri sana ila si lazima uchangie na clouds nao lazima waache unyonyaji?
 
Clouds wanawa exploit kivipi wasanii? Unaweza ukatoa maelezo yenye vielelezo?[/e QUOTE]
Ndo umetumwa nn-sina singl
e inayoruka hewani mm

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ok ngoja nitoe ufafanuzi kidogo juu ya hili, Huwa sipendi kuona anayeuliza anakosa ufafanuzi.

Kwanza sidhani kama wasanii wamekuwa ombaombam kwa sababu zifuatazo:-

Ni wao wasanii wenzake na marehemu ndio wametamani kuendesha mazishi yenye hadhi fulani kwa ajili ya
mwenzao na wameomba mashabiki nao washiriki kwa michango ili lengo litimie na sio kwamba bila ya hiyo
support mazishi yatashindikana.

Pili sidhani kama kunakosekana wasanii au wadau wanaoweza kubeba shughuli hii yote, wanachofanya ni
kushirikisha wengine, sioni kama huku ni kuomba omba.

Tatu, wapi imeandikwa kwamba ukishakuwa msanii tu basi lazima uwe milionea, Sijui kuhusu marehemu lakini
usanii ni jambo moja na kuwa milionea ni jambo lingine.
 
Kuhusu wasanii kunyonywa, hasa na hawa clouds.....naungana nanyi kabisa kwenye hili.

Nani asiyekumbuka jinsi wasanii walivyokuwa na maisha mazuri kabla ya ujio wa clouds wanyonyaji. Enzi za redio adilifu RTD. Wasanii kama marehemu Marijani, Mbaraka, Balisidya, Niko zengekala na wengine waliona matunda ya kazi zao. Vipi kama clouds wangekuwepo enzi zile. Pia tukumbuke ujio wa REDIO MOKO chini ya watangazaji mahiri Mzee Chaz, Nyaisanga na wengine, jinsi walivyoibuka wasanii kama Muumini(kocha wa dunia), Banza (mwalimu wa walimu), Mhina Panduka(Toto Tundu), Omary mkali, Misambano, Sonyo na wengineo, jinsi walivyofaidi manufaa ya kazi zao kwa kuwa tu haya majamaa ya clouds hayakuwepo. Juzi nimesikia eti Diamond ana bilioni moja tu kwenye akaunti. Wizi mtupu.....Diamond ni wa kuwa na hela chache hivyo kweli...Na ukiona hivyo ujue clouds wamepiga bilioni moja kutoka kwake. Tuungane tuitokomeze clouds tuone matunda ya muziki wetu. Turudi enzi za RTD, Redio moko n.k. Mtafaidi kama walivyofaidi kina Bichuka, Dede, Ngurumo, Zahiri Zoro,Bakule, Ndada na wengine.........Eti Diamond ana bilioni moja...Tuing'oe clouds muone akaunti za kina mzee Makasy, Tongolanga,Chimbende ....zitakavyosoma.

KUJIUNGA NA HARAKATI HIZI WASILIANA NA MH MISTA MBILI.
 
Wasanii ni sikio la kufa huenda likasikia
kwa Mungu.
 
Sorry nilitaka kusahau, Hata mkiwasiliana na profesa au Dada mtakuwa mmejiunga na harakati hizi maalum za kumkomboa msanii.

Msimamo wetu ni kwamba:-

TUNATAKA KUBAKI NA RADIO AMBAZO HAZINYONYI WASANII NA WALA WASANII HAWAPATI...oooh sory..NA WALA

WASANII HAWANYONYWI.........


NI BORA TUKOSE WOTE....oh shit..hayo maneno ya chini usisome...hayahusiki...
 

Hayahusiki....,
tuneyanote na tushajua unachokimaanisha hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…