Ryzen
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 7,301
- 8,706
Habari za usiku,
Nisiposema hili nitalaaniwa hata, Katika makuzi yetu kwa Namna moja ama nyingine tumeweza kuwakosea wazazi wetu hasa kina mama..
Hawa mama zetu ukiwakosea wanakimbilia Haraka Kulaani, Leo nikiwa napita Mtaa mmoja Nilisikia Dirishani kwenye Nyumba za Kupanga Mama Mmoja akimuadhibu kwa fimbo binti yake ambaye yupo shule ya Msingi na kwa mazungumzo yao Nadhani Binti yupo darasa la Nne..
Binti huyu anaadhibiwa kwa fimbo randomly kwa sababu ya kuficha makaratasi ya matokeo yake ambayo mama yake anahisi amefeli..Kilichonisikitisha ni lugha alokuwa akitumia Mama yake lugha iliyokaa kama kumlaani na maneno kama Sugu, Jambazi na hata kumlalamikia Mungu kwanini kampa mtoto kama huyo..
Hii ikanikumbusha mbali, enzi hizo mama yangu pia alikuwa akitumia maneno ambayo kweli mzazi hupaswi kumtamkia mwanao maana hayabariki, Maneno kama Kumuita mwanao Jambazi,Malaya,Muhuni au hata kumlaumu Mungu kwa aina ya Mtoto wako na mengine mengi ambayo kwa kweli hayabariki!
Mara Pengine Ndugu wazazi haya maneno yenu huumba, unamtamkia mwanao maneno maovu na yasiyobariki mwisho wa siku akiishia kubaya ni sawa na wewe umemlaani na akiharibika ni matokeo ya laana yako na atakuwa mzigo wako tena.
Ndugu wazazi Nashauri Mwanao anapokosea kwanini usiseme hata Kimoyomoyo ya kwamba Mungu amsamehe kwa kuwa hajui atendalo na amjalie aindee njia iliyo sawa?
Tujifunze.. zama zimebadilika..Zungumzeni kwa upole na busara na Wanenu kuliko kuishia kuwapa maneno yasiyobariki!
Mungu Mwenyezi Awajalie Usiku Mwema!