Kitendo cha Kampuni ya simu za mkononi ya zantel kulazimisha wateja wao wa modem wanaolipia malipo ya internet kwa malipo ya kabla kupitia huduma ya/za Z-Mono na nyinginezo kwa ajili ya matumizi ya mwezi na ikatokea mtumiaji wa huduma hiyo kumaliza matumizi ya megabytes alizopewa kabla ya mwezi na akataka kulipia tena huduma hiyo kukataliwa kufanya hivyo siyo sahihi. Mteja anapomaliza megabytes alizopewa kabla ya muda analazimishwa kununua huduma nyingine yenye bei kubwa zaidi kuliko aliyotumia mwanzo. Kwa kitendo hiko ni wazi kuwa mnajikosesha mapato mengi kwani kwa wateja walio wengi wataacha kutumia hizo modem hadi kipindi alichozuiliwa kimalizike. Na ikumbukwe kwamba hata watumiaji hao wa internet wana uwezo tofauti wa fedha hivo siyo sahihi kulazimisha mtu kununua huduma ambayo hana uwezo nayo wa kuilipia.