KERO Kwa hilo la barabara ya Lusahunga hadi Rusumo Serikali inacheza na hatari!

KERO Kwa hilo la barabara ya Lusahunga hadi Rusumo Serikali inacheza na hatari!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

alexelias

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2017
Posts
2,032
Reaction score
3,197
Tumelizungumza sana hilo jambo la angalau barabara ile irekebishwe kwa kufukiwa mashimo makubwa lakini hakuna hatua yeyote inayochukuliwa na barabara imekuwa mbovu kupindukia!

Ikumbukwe barabara hiyo ina maeneo hatarishi sana kwa uhalifu hasa maeneo ya Ngazi Saba hadi Milima ya Nyabugombe.Ubovu wa barabara ile hasa maeneo hayo yanarahisha sana wahalifu kufanikiwa kufanya uhalifu wao kwani malengo yao yatarahishwa na ubovu wa barabara ile kwa magari kwenda taratibu ya hadi kiwango cha mwendo wa 5km kwa saa.

JANA KWA MFANO ENEO LA NYABUGOMBE LILIKUWA HALIPITIKI KWA SABABU YA UBOVU NA MAHANDAKI YALIYOPO KATIKA barabara ile.

Wiki iliyopita pia barabara hiyo hiyo eneo la Nyabugombe ndogo hadi Nyakahura barabara ilikuwa haipitiki.

Itoshe kusema,Serikali yenyewe inakaribisha uhalifu kwa kuandaa mazingira rafiki kwalo.

Tabia hii ya Mamlaka kufumbia macho mambo nyeti kama hayo na kuja kusababisha matatizo baadae imekuwa ikijirudia sana.Ni mda mwafaka sasa kwa Mamlaka kuitazama na kuifanyia ukarabati mkubwa barabara hiyo.
20230219_131550.jpg
20230219_131546.jpg
20230219_131544.jpg
20230219_131541.jpg

Picha juu ni barabara ya Biashara inayounganisha Tanzania na Nchi za Rwanda na Burundi Eneo la Lusahunga -Benaco. 21% ya mzigo kutoka Bandari ya Dar unapita hapa.


Pia Soma; Sasa barabara ya Lusahunga – Rusumo yenye urefu wa kilomita 92, kujengwa kwa Bilioni 153
 
Back
Top Bottom