Kwa hivi karibuni kuna kizazi cha hovyo kinachoongezeka

Kwa hivi karibuni kuna kizazi cha hovyo kinachoongezeka

Cecil J

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2023
Posts
434
Reaction score
1,024
Gwala kwa wana Jf.

Niteremke hapa kwenye ngazi taratibu na kuingia kwenye mada.

Makuzi ya miaka ya sasa imepelekea kupatikana kizazi cha hovyo kweli! Watoto kutojua wanapaswa kuongea vipi na watu mbalimbali, mfano watu wazima, waliowazidi vyeo, na mengine mengi. Yaani mtoto anaongea na mtu mzima namna ile ile anavyoongea na rafiki yake wa miaka 15 🤣🤣

Sijui ni mfumo au nini, vijana wakiume wa sasa wanaishi maishi nyoro nyoro sana, kijana wakiume anakubali kuwa mtekemteke, kazi hataki, akiipata kazi anafanya kwa kujisikia. Bahati mbaya vijana wa kiume wanaobinua midomo huko TikTok nao wameongezeka.

Vijana kwa upande wa wakike na wakiume kwasasa kuwekeza kwenye Elimu na Ujuzi ni kama science ya akina Keppler, Newton, Leibnitz, Galileo, Webber na wengine wanaoendana na hao. Vijana wanajisikia vizuri kutojua chochote zaidi ya muvi, miziki na starehe, 🍷🍺 kamnyweso kwa sana lakini kichwani hamna kitu.

Unakutana na kijana mhitimu wa kozi ya Uhandisi wa computer, cheti anacho, GPA yake inaridhisha mno kapiga 4.0 na kuendelea, ila limetokea tatizo dogo ofisini labda la kupiga windows anadai anajua kupiga window mwisho wa siku anafuta docs zote na kubebesha windows.

Kijana anamiliki smartphone na hata kuandaa business plan hawezi, kapata 1M ya mazabe anazama google na kupitia biashara kadhaa, wiki haijapita anazaba 1M yote.

Aisee, it 's too much.

Vijana amkeni, mjifunze kujisaidia kwanza. Elimu yenu iwe yenye maarifa na Utashi.
 
Kwanza ulivyoanza tu kwa salama ya GWALA sijaendelea kusoma maana nmejua moja kwa moja ww nae ni miongoni mwa vijana hao wa hovyo
 
Back
Top Bottom