Nimekutana na clip hii huko duniani na nimepata maswali sana
Nimeona kuna huyu jana kashika bango akiwa anataka kile kilichofanyika kule Venezuela kifanyike huko huko South Africa.
Yaani kaenda kuchongesha bango kabisa yuko mtaani anaomba Trump aichukue South Africa. Niwakumbushe wakuu, haijapita hata miaka 40 tangu Mzungu afukuzwe Afrika Kusini, leo watu wako barabarani wanataka Ramaphosa abebwe, Marekani iichukue Afrika Kusini.
Nimeona pia the same calls hapa Tanzania baadhi ya watu wakitaka Marekani ije ifanye kile cha Venezuela in exchange tutawapa madini.
Sasa nauliza wakuu, hii ndio tumeamua kuwa suluhisho ya matatizo yetu?
Kosa kubwa sana ambayo waafrika tulifanya na ambayo itatugharimu milele ni kudai uhuru wakati hatukupewa kipawa cha kutawala na ndio maana pamoja na rasilimali zote tulizonazo bado sisi ndio jamii ya watu fukara zaidi duniani.😩😩😩
Africa inasikitisha sana. Wala hatuweki efforts zozote za maana za kuendeleza bara hili
Mpaka leo tunadili tu na usambazaji wa huduma za kijamii huku kila bidhaa tunaagiza kutoka nje. Hatuna hata kampuni kubwa ya kututangaza kimataifa. Dah.... Afrika inasikitisha sana