Kwa hizi views YouTube, Mbosso anakuja juu zaidi ya Aslay...

Dong Jin

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2018
Posts
968
Reaction score
2,034
Wote mwezi uliopita (mwezi wa 9) waliachia video za ngoma zao pendwa... Alianza aslay akaachia video ya Kwatu tar. 12/9 (takribani siku 46 zimepita).... siku kumi na nne baadae yaani yar. 24/9 Mbosso naye akaachia video ya Hodari (Takribani siku 32 zimepita)...
Lakini kwa jinsi views zilivyo katika mtandao wa utube inaonesha kabisa mbosso kamfunika mwenzake mbali mnooo
Kwatu mpaka sasa ina views milioni 1.4 na ushee..
Wakati Hodari ina views milioni 2.9 na ushee... licha ya kutofautiana muda wa kuachiwa
Toa maoni yako kama unaamini Aslay keshazidiwa na Mbossokhan mshedede
 
Kila mmoja ana uwezo wake. Ndio maana yule akaitwa aslay na huyu akaitwa Mbosso, hawalingani kwa lolote!
Wote wapongezwe kwa kujibidiisha katika talanta zao na si vinginevyo
 
Hivi kwanini bingo views huwa inaonekana kushadasiwa sana wakati akina Justine bieber wanapiga Views billion 1 Halafu hana muda nazo kabisa?

Kuna vitu vingine huwa tunalazimisha kuvitengenezea mazingira ambayo sio hii kitu ilikuwa sio ya kuianzishia thread
 
Hivi kwanini bingo views huwa inaonekana kushadasiwa sana wakati akina Justine bieber wanapiga Views billion 1 Halafu hana muda nazo kabisa?
Bongo ubora wa wimbo unapimwa na views za UTube
 
Hivi kwanini bingo views huwa inaonekana kushadasiwa sana wakati akina Justine bieber wanapiga Views billion 1 Halafu hana muda nazo kabisa?
huyo chris brown tu anashadidia views,icjekuwa wabongo!
 
Bongo ubora wa wimbo unapimwa na views za UTube
Sio ubora wa wimbo, ni umaarufu wa wimbo na kukubalika kwa wimbo

Na ni dunia nzima,

YouTube views is the New Billboards charts
 
Mboso mimi na shida na meneja wake tu


Kadada kazur, kadogo afu smart
 
Naona Mboso anaichukua nafasi ya Aslay.... - JamiiForums
 
naona unampa promo mzee wa kusafisha mtaro
 
Mimi nawaelewa wote wawili ila kiukweli Kwa kipaji na ubora wa tungo, ASLAY ni bora zaidi ya Mbosso. Ila kinachotokea kwa sasa ni kuwa MBOSSO ana Back-up kubwa sana ya WCB wakiingozwa na Mondi hususani kwenye promotion na Marketing.
Kwa mfano nyimbo ya HODARI ni nyimbo ya kawaida sana ukiangalia Melodia yake na Lyrics zake ila tu imekuwa highly promoted ndio maana iko hivyo.
MAWAZO YANGU.
 
Hodari iko na vichombezo adimu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…