Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Marufuku imekuwa ikipigwa na madhehebu ya walokole , hasa kwa wanawake ambao wanapo okoka wanakuwa tayari wana watoto lakini hawana ndoa ama kwa kifupi wamezaa kabla ya ndoa.
HOJA ZA WANAOPINGA SEND OFF/K-PARTY:
HOJA ZA WANAOPINGA SEND OFF/K-PARTY:
- Wewe binti, kishakula tunda la mti wa kati , amekaa kwa mwanaume miaka 4 yote akiwa chuo, kazalishwa alafu kaachwa kaja kuolewa eti anaenda kanisani kufundishwa ndoa na mtu aliyezuiliwa kuoa kwa sheria za Wazungu. Huu ni ujinga wa hali ya juu kwakuwa huyo anayekufundisha hajui lolote.
- Binti umekaa kwa mwanaume , Hamisa ameishi na Aziz K miaka 3 sasa, alafu jumamosi hii eti Send off, yaani aagwa wapi wakati alishajiaga mwenyewe?
- Send of kufanyikia ukumbini, wakati mtoto anaagwa nyumbani kwao, huu ni ujinga.
- Mwanamke umeshatoa mimba zaidi ya 5 ukiwa chuo, alafu unataka baby shower ya mwanao, vipi hao 5 ulioua?
- Wanataka waweke historia kwenye familia, kumbuka sensa inaonyesha kwenye familia ya watoto 5 wa kike, mmoja ndio huolewa akiwa bikra na akitokea nyumbani, wengine hujisogezza na kuazalia huko.
- MICHANGO-mwanamke amechangia ndoa za wenzie tangu kuanza kazi mpaka kifua kimelegea na yeye kapata mtu wake aliyechoka sasa anataka achangiwe.
- MITANDAO YA KIJAMII:-wanawake wengi wanataka hizo send of na baby shower ili wapate cha kuposti na kuwakera ma-ex wao.