Kwa huu mgogoro wa CHADEMA itabidi tuendelee kupenda mpira na story za tunda kimasihara

Kwa huu mgogoro wa CHADEMA itabidi tuendelee kupenda mpira na story za tunda kimasihara

uhurumoja

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Posts
9,616
Reaction score
22,521
Kwa muda mrefu sana toka wakati wa Chacha Wangwe, Zitto n.k CHADEMA kimekuwa chama rigid na kisichokubali kabisa kukosolewa hasa kupitia wafuasi wake ambao ukijaribu kukosoa utashambuliwa sana. Sasa kwa wale wanaojua siasa za nchi hii chadema ndio inazama.

Yah, kama jua la jioni upande wa Magharibi CHADEMA ndio inazama. Kama vilivyo vyama vingine rangi za majengo na bendera vitabaki kama alama kwa angalau miaka 10 ijayo Kisha vitafutika rasmi kama NCCR.

Kwa sasa ngoja tungoje Euro huku tukifurahia mbilinge za usajili.
 
Fikra za mwenyekiti .......weeee ziendelee kudumu milele na milele.

Mwalimu JK Nyerere aliwahi kusema na kuwashauri wanasiasa wengine wakati "akingatuka" alisema ni vyema ukaondoka ukiwa bado watu ama wafuasi wako bado wanakupenda.........

Namshauri Mwenyekiti Mbowe azingatie wosia wa BABA wa Taifa letu. ng'atuka wakati bado wanachama wako wanakupenda.
 
Kwa muda mrefu sana toka wakati wa Chacha Wangwe, Zitto n.k CHADEMA kimekuwa chama rigid na kisichokubali kabisa kukosolewa hasa kupitia wafuasi wake ambao ukijaribu kukosoa utashambuliwa sana. Sasa kwa wale wanaojua siasa za nchi hii chadema ndio inazama.

Yah, kama jua la jioni upande wa Magharibi CHADEMA ndio inazama. Kama vilivyo vyama vingine rangi za majengo na bendera vitabaki kama alama kwa angalau miaka 10 ijayo Kisha vitafutika rasmi kama NCCR.

Kwa sasa ngoja tungoje Euro huku tukifurahia mbilinge za usajili.

Waroma wana msemo wao kwamba ili kuwatoa wajinga kwenye mambo muhimu yanayohusu maisha yao na kuendesha nchi tafuta vitu ambavyo vita preoccupy na kuwaweka bize akili zao. Vitu hivyo ni mpira na mashindano mbalimbali, kamari/betting etc... Hivi vitawafanya wawe bize muda wote, ikiisha ligi moja wanahamia nyingine na nyingine etc huku wakiwa hawana muda wa kuhoji mambo muhimu ya nchi yao, maisha yao na mustakali wa maisha yao na vizazi vyao.....Kalagabahoooo....
 
Back
Top Bottom