Bajeti ya kunguru
JF-Expert Member
- Sep 21, 2014
- 1,379
- 1,069
Wasalaam waheshimiwa mawaziri, waziri wa kazi,ajira, vijana na walemavu mh. Jenister Mhagama na waziri wa elimu sayansi na teknolojia mh. Prof. Joyce Ndalichako. Awali ya yote ninayo furaha kutoa pongezi zangu kwenu kwa uteuzi mlioupata, ni kwamba mpaka sasa taifa lina matumaini na mategemeo makubwa kutoka kwenye utendaji wenu na usimamizi wenu. Nisiwachoshe kwa salamu naomba niende moja kwa moja kwenye kusudio la pili la kalamu hii.
Tanzania kwa sasa si miongoni mwa nchi maskini ulimwenguni, kutokana na hatua hii nzuri tuliyopo tumeanza kupata heshima walau kidogo kwa kuvuka sifa za kinachoitwa misaada kwa nchi maskini, ambayo ni hatua kuelekea heshima kamili ambayo tunastahili kuwanayo.
Maendeleo ya nchi yana uwanja mpana wa kuyaelezea katika njia kuu zake mbili KIBEPARI na KIJAMAA. Changamoto kubwa ni kuwa makundi yote huwa yamo ndani ya kila taifa ila kwenye kipaumbele cha taifa ndipo kundi moja hulazimishwa ku surrender.
Ni wazi akili na mioyo ya watanzania waliowengi ipo ki mfumo wa ujamaa,unaweza ukasema ni wavivu lakini hakuna ukweli, wengi hutegemea serikali ndiyo yenye mamlaka na maamuzi ya mustakabali wa maendeleo ya maisha yao na vijana wao.
Kutokana na mantiki hiyo ilijengeka ndani ya jamii yetu watanzania, kuna sehemu imeonekana mambo yamesimama. Hakuna ubishi idadi ya wananchi inazidi kuongezeka kila uchwao. Kuongezeka kwetu Sio mzigo bali ndio utajiri wetu.
Jitihada za kuongezeka kwetu zipo, jitihada za kuwasomesha watoto wetu zipo ila tatizo linakuja kutokuwa na lengo la kumtegemeza kijana tuliyemsomesha ili awe na uwezo wa kujitegemea na kurudisha mchango serikalini wa gharama zilizotumika kumuwezesha.
Kama nilivyoeleza awali,jamii ya watanzania inamizizi ya mfumo wa kijamaa, mfano pale serikali ilipoamua elimu ya sekondari ikuzwe/iboreshwe ili kufanya watoto wengi waweze kuipata, watanzania waliitikia na hata pale walipokwama gharama serikali iliwasaidia mpaka sasa tupo kwenye mfumo wa elimu bure. Haihitaji kueleza kinaga ubaga watanzania tulipata mshangao wa namna gani na faraja kiasi gani kutoka kwa serikali yetu (hivi ni viashiria vya ujamaa ndani ya mioyo ya watanzania).
Baada ya kuwasomesha watoto wetu wanaturudia majumbani kukaa huku wakiwa na matumaini ya ajira na miaka inazidi kwenda. Hapa kuna tatizo la kiufundi. Haiwezekani serikali iendelee kula hasara kwa kuwasomesha watoto wetu na kuwaacha tu hivi hivi. Turudi kwenye makini zetu, kila jambo tunalolifanya tujue namna ya kupata return chanya yake, tusiendelee kufanya jambo ambalo hatujauandaa mwisho wenye manufaa.
Maoni yangu binafsi ni kuwaunganisha nyie wawili muweze kutuletea mfumo wa elimu ambao utakaolazimisha elimu ya ufundi/ujuzi kuwa ya lazima kwa kila mtoto atayeshindwa kuendelea na masomo ya sekondari. Madhumuni ya mfumo huo uwe ni
(i). Kurudisha gharama za serikali zilizotumika kuwaelimisha watoto wetu kwa kuchukua asilimia fulani ya mapato watayoyapata kutokana na shughuli za ujuzi walioupata.
(ii). Kuwategemeza watoto wetu watuondokee majumbani. Mtoto/ kijana anapokuwa na ujuzi fulani anakuwa anauwezo hata wa kupata senti kadhaa hivyo atakuwa na hamu ya kutoka kwa wazazi wake na kwenda kuanza maisha yake (jeuri ya pesa).
(iii). Utulivu wa jamii yetu kama watanzania. Vijana wengi ambao hawana ajira wengi wao hujikuta tena hawana familia (kuoa/kuolewa) hivyo huwa wanakuwa watu rahisi kuwashawishi katika mambo ya uvunjifu wa amani kwani huwa hawana jasho la kulilinda.
Kuna faida nyingi zitazopatikana kutokana na kurekebishwa kwa tatizo hilo la kiufundi.
Nyinyi ndio mpo hapo juu na mnaona kwa mapana zaidi tofauti na mimi ila wote dhumuni letu kubwa litabaki lile lile KUIJENGA TANZANIA MOJA.
Nawasilisha.
MAGUFULI4LIFE.